Loading...

KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI.

Loading...
KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI.
link : KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI.

soma pia


KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI.

Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.


Desemba 02, 2018 ilitimia miaka mitatu tangu mwanamuziki Kasongo Mpinda ‘Clayton’, aliyefariki Desemba 02, 2015 akiwa nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya Kisukari.

Mwanamuziki huyo alitamba katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi humu nchini zikiwemo za Maquis du Zaire na baadaye MK Group, kabla ya kujiunga kufanya kazi ya muziki na gwiji la muziki nchini, Kikumbi Mwanza Mpango Mwema Kyembe ‘King Kiki’ na kundi lake la La Capitale ‘Wazee Sugu’.


Kasongo aliingia nchini Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1970 akiwa na bendi ya ‘The Wings Brother’s’ aliyoianzisha mwenyewe akiwa huko kwao Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akiambatana na wanamuziki wa bendi hiyo walisafiri wakitoka katika nchi za Zambia, Botswana na Zimbabwe hadi humu nchini kutoa burudani.

Mwaka 1979 akaangukia mikononi mwa bendi ya Maquis du Zaire iliyokuwa ikiungurumisha muziki katika ukumbi wa White House, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kasongo aliweza kuzikumbuka baadhi ya nyimbo alizotunga au kushiriki kuimba akizitaja nyimbo alizotunga na kuimba akiwa Maquis du Zaire za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine kibao.

Kasongo Mpinda  ‘Clayton’ akisaidiana na Mbombo wa Mbomboka,  walikuwa waanzilishi wa bendi ya MK. Group iliyokuwa ikifanya vitu vyake katika ukumbi wa Bandari Grill aliyopo katika hoteli ya New Africa, katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Akiwa na bendi hiyo iliyokuwa ikitumia mtindo wa ‘Ngulupa’ alifanikiwa kuifanya kuwa ya kipekee kuanzia upigaji hadi utaratibu wa kimahudhurio kwa upande wa wapenzi na mashabiki.

Mpinda kuna wakati aliwahi kutetea kuwa muziki wa dansi umeshuka akisema kwamba  kuwa muziki huo hauwezi kushuka kutokana na kwamba una tabaka lake mahususi kiushabiki.

Alisema hata vijana wa sasa wanaoonekana kuishabikia Bongo fleva, itafikia kipindi watalazimika kuwa mashabiki wa dansi kutokana na umri wao kuwaruhusu.

Aidha Kasongo Mpinda aliweza kuonesha makali yake akiwa na bendi ya Zaita Muzika aliyojiunga nayo baada ya miaka minane ya kuitumikia MK Group.

Wakati akiwa hai  wake aliwahi kufanya mazungumzo na mwandishi wa habari hizi, akaeleza kuwa alizalliwa Februari 2, 1945 Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanane unaotokana na ukoo wa ki Chifu.

Baba wa Babu yake alikuwa akiitwa Chifu Kasongo huko Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baba yake mzazi mzee Boniface Mpinda Kasongo, alikuwa mfanyabiashara maarufu katika mji wa Lubumbashi, wakati mama yake Kanku wa Mokendi, alikuwa muumuni na mwimbaji mashuhuri katika  Kanisa la kikatoliki mjini humo.

Mpinda alibainisha kwamba mama yake ndiye aliyekuwa chanzo cha yeye kupenda kuimba kwa kuwa kila mara alikuwa akifuatana nae kwenda Kanisani kuimba.

 ‘Clayton’ hakuweza kuendelea na masomo ya  sekondari baada ya wazazi wake wote  kufariki dunia akiwa kidato cha kwanza.

Safari yake ya muziki ilianza katika bendi ya Ode Jazz na baadae akajiunga katika bendi ya Lupe Jazz, zilizokuwa Lubumbashi.
Mwaka 1965 Kasongo alikwenda katika jiji la Kinshasa kutafuta bendi ya kujiunga nayo, ambapo alikutana na Dokta Nico Kasanda, aliyekuwa mmiliki wa bendi ya L’Africa Fiesta Sukisa.

Alipiga muziki na bendi  hiyo hadi mwaka 1968,  alipoachana na Dokta Nico akaamua kuvuka mpaka akaingia mji wa Lusaka nchini Zambia.

Mwaka uliofuatia wa 1969 na kuanzisha bendi yake ya The Wings Brother’s,  mjini Lusaka.

The Wings Brother’s ilijumuisha vijana toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliokuwa wamechipukia katika  muziki wakati huo.

Aliwataja kuwa ni akina Kibambe Ramadhani, Lomani, Jozee, Lushiku wa Lushiku na Kayembe Trumbloo.

Chini ya uongozi  wake bendi, hiyo ilisafiri kwenda kupiga muziki katika nchi za Botswana, Zambia hatimaye wakatua hapa nchini Tanzania mwaka 1979.

Haikuchukua kipindi kirefu ambapo yeye na baadhi ya wanamuziki wenzake walijiunga na bendi ya Maquis du Zaire, huku wanamuziki wengine wakijiunga na bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS).

Baada ya ujio wa vijana hao kukawa na ushidani mkali kati ya bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS) iliyokuwa ikipiga muziki wake kwenye ukumbi wa Kimara resort na Maquis du Zaire iliyokuwa imejikita ukumbi wa White House Ubungo.


Kasongo alifunga ndoa ya kiisilamu na Bi. Habiba mwaka 1984, jijini Dar es Salaam. Kabla ya kufunga ndoa hiyo, alilazimika kuingia dini ya kiislamu,  hivyo alisilimishwa na kupewa jina la Abubakar.
Katika maisha ya ndoa yao walifanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Johari, Kiloman, Mpinda na Idd.

Kati yao wawili ndiyo waliofuata nyao za baba yao ambapo  Idd ‘Clayton’ yupo katika kikosi cha Twanga Pepeta Academy akifanya vizuri katika muziki wa dansi na  Kiloman anapiga muziki wa kizazi kipya.

Kwa muda mrefu Clayton hakuwa vizuri kiafya kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Kisukari na ngazi yaliyohitimisha safari yake ya kuishi duniani.

Kabla ya hatma yake kimuziki alikuwa akifanya kazi ya muziki katika bendi ya La Capitale ‘Wazee Sugu’ akiwa pamoja na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ na  baadae alijiunga na bendi ya Bana Maquis inayoongozwa na Tshimanga Kalala Assosa.

Boubakar Kasongo katika mazunguzo yake aliwahi kutamka kuwa alikuwa akiona raha kuimba pamoja na marehemu Issa Nundu ‘Prince’.

Alisema kuwa ukiwaondoa Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ na Tshimanga Assosa, mwimbaji pekee aliyekuwa akimpa changamoto kubwa enzi za Marquis na MK Group ni mtunzi na mwimbaji mahiri Hassan Rehani Bitchuka.

 “Nasikitika nimekuwa masikini licha ya kutumika sana huko nyuma, hii ni kutokana na kuchelewa kwa mafanikio ya kimuziki hapa nchini, lakini ingekuwa ni kama sasa, muda huu mimi ningelikuwa tajiri kama msanii Diamond…” alisema Clayton enzi za uhai wake.

Akiwa kama mkongwe katika tansnia ya muziki wa dansi Aboubakar Kasongo Mpinda aliwahi kutoa usia kwa wanamuziki wa dansi kutokata tamaa pamoja na kushirikiana.

Alisema kuwa mawazo ya wengi kwenye ushirikiano huzaa kitu kizuri na kwamba ubinafsi ndio unaosababisha nyimbo nyingi za sasa kuwa na ubora muda mfupi.
ABOUBAKAR KASONGO MPINDA 'CLYTON' (L)AKIIMBA SAMBAMBA NA ISSA NUNDU



Hivyo makala KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI.

yaani makala yote KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kasongo-mpinda-aliyekuwa-gwiji-wa-muziki.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI."

Post a Comment

Loading...