Loading...
title : KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI
link : KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI
KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI
Na Moshy Kiyungi.
Mnamo miaka ya 1970 hadi 1980, sauti ya mwanamuziki Kasongo wa Kanema ilikuwa ikisikika kwenye redio nyingi Afrika ya Mashariki.
Sauti yake ilitawala hususan kwenye wimbo wa Kakolele Viva Krismasi, wakati akiwa katika bendi ya Baba Gaston.Kasongo wa Kanema alianza shughuli za muziki akiwa na umri mdogo wa miaka kumi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Nguli huyo alikuwa akichukua muda mwingi akisikiliza nyimbo za wanamiziki mahiri katika uimbaji akina Tabu Ley naLuambo Makiadi Lokanga la dju Pene Francois ‘Franco’ambaye pia alijulikana kwa majina maarufu ya Franco Yogo au Le Grand Mitre.
Familia ya Kasongo haikuwa nyuma kumpa moyo kwa kiasi kikubwa wa kufanya muziki. Kipaji chake kilionekana pale alipoungana na wenzake kuunda bendi ya Super Mazembe. Baadhi ya wanamuziki hao walikuwa akina Atia Joe, Lovi Longomba, Bukalos Kayembe Rapok, Songole, lobe Mapako, Talos, Longwa Didos na Fataki Lokasa ‘Masumbuko ya dunia’.
Kwa mapenzi ya mungu, baadhi yao wameshatangulia mbele za haki.
Walio hai ni yeye Kasongo wa kanema na Dodo Dorris, ambaye hivi sasa anaishi nchini Afrika ya Kusini. Akiwa katika bendi ya Baba Gaston iliyokuwa ikiongozwa na Baba Nationale Omar Ilunga wa Ilunga, Kasongo wa Kanema alijijengea umaarufu zaidi alipoimba wimbo kwa umahiri mkubwa wimbo wa Kakolele Viva Krismas.
Wimbo huo kila ikaribiapo nyakati za sikukuu ya Krismasi, hurindima takriban katika vituo vingi vya redio.Baadaye Kasongo akatoka kwa Baba Gaston akaenda kujiunga katika bendi ya Super Mazembe.
Alishiriki vilivyo kuimba nyimbo nyingi katika bendi hiyo ya Super Mazembe akisaidiana na watunzi na waimbaji wengine akina Lovy Longomba na Fataki Lokassa ‘Masumbuko ya duniya’.
Walishirikiana vilivyo kutunga na kuimba nyimbo kama Bambina, Shauri yako, Likasi, Bamama, Mukala, Loboko na nyingine nyingi.Aidha Kasongo wa aliwahi kupigia katika bendi ya Shika Shika, ambako nako aliimba kwa umahiri mkubwa katika nyimbo za Maya na Nyako Ber.
Akiwa na bendi hiyo ya Shika Shika alikutana na mwimbaji Fumimoto Jimmy Moni Mambo, kwa pamoja waliweza kuchanganya sauti zao na kuifanya bendi hiyo kuwa tishio katika jiji la Nairobi miaka hiyo.
Kanema baadae akaamua kuunda bendi yake ikiwa na baadhi ya wanamuziki mahiri akiwemo yeye kama mwimbaji kiongozi na kiongozi wa bendi, mwanaye aitwaye Kasongo jnr. ambaye alikuwa akiimba na kubofya kinanda.
Wengine ni Ale Maindu ambaye alikuwa akicharaza gitaa la solo, Lei Mkonkole, akichangaya drums na Longwa Disco, aliyekuwa mwimbaji. Gitaa la kati rhythm na solo yalikung’utwa na Alpha Nyuki.
Kasongo wa Kanema amefaya makazi yake katika jiji la Nairobi nchini Kenya. Ni baba wa familia yenye mke aiitwaye Achieng na watoto kadhaa.
PICHA YA KASONGO WA KANEMA (KULIA), AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI MJINI NAIROBI.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 0713331200, 0767331200 au 0784331200.
Hivyo makala KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI
yaani makala yote KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kasongo-wa-kanema-aliyetisha-kwenye.html
0 Response to "KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI"
Post a Comment