Loading...

MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA

Loading...
MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA
link : MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA

soma pia


MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA


MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka, Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Thuwayba Kisasi, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo wakipewa maelezo na Mhandisi Abubakar Khamis Mati juu ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya Kisasa ya Sekondari ya Wara iliyojengwa na SMZ kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki shughuli za ujenzi wa Tawi la CCM Kangani ambalo ni Tawi la asili la harakati za ASP linalojengwa upya ili liendane na hadhi ya CCM.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki shughuli za ujenzi wa Tawi la CCM Kangani ambalo ni Tawi la asili la harakati za ASP linalojengwa upya ili liendane na hadhi ya CCM.

……………………………………………………………………..

NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.

WANAWAKE wa Chama Cha Mapinduzi kisiwani Pemba wametakiwa kufanya Mapinduzi ya kisiasa kwa kuhakikisha CCM inavunja na kusambaratisha ngome ya CUF na hatimaye kushinda majimbo yote ya Uchaguzi ya mwaka 2020.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka katika mwendelezo wa ziara yake huko Shule ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, alisema ni wakati wa wanawake kuonyesha uwezo wao na kutekeleza kwa vitendo falsafa ya ‘Wanawake ni jeshi la ukombozi la CCM’.

Alisema hakuna chama cha siasa, wala taasisi yoyote itakayoweza kuzuia ushindi wa CCM mwaka 2020 kisiwani Pemba endapo wanawake wataamua kuungana kwa pamoja ili kufanikisha ushindi wa CCM.

Katika maelezo yake Ndugu Gaudensia alisema Jeshi la UWT la Chama Cha Mapinduzi litakuwa mstari wa mbele kupambana vita ya kisiasa kwa mbinu zote ili kuandika historia mpya katika uwanja wa siasa za ushindani Tanzania kwa kuhakikisha CCM inashinda kwa kiwango kikubwa Zanzibar na Tanzania bara.

“Wanawake tuna nguvu, uwezo, ujasiri, mikakati,nyenzo na mbinu za medali za kisiasa hivyo hatuna sababu ya kuyaachia majimbo ya Pemba yaendelee kubaki kwa wapinzani bali yatarudi mikononi mwa CCM.”,alisema Bi.Gaudensia.

Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia, alipongeza hatua za kimaendeleo zilizofikiwa katika Sekta ya Elimu Pemba hasa katika suala zima la miundombinu ya Majengo ya Kisasa ya kiwango cha Ghorofa.

Aidha aliyataja mageuzi makubwa katika miundombinu ya Barabara za kisasa mijini na Vijiji kuwa ni ya kiwango bora cha kuridhisha hatua ambayo wananchi wa kisiwa cha Pemba wanastahiki kuithamini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo mema yaliyotekelezwa.

Pamoja na hayo aliwasisitiza hakina Mama Visiwani Pemba bila kujali tofauti zao za kisiasa kushiriki katika kongamano la Kitaifa litakalofanyika Machi 9 mwaka 2019, katika Kiwanja cha Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Alieleza kuwa Kongamano hilo lililoandaliwa na UWT ni la kupongeza utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 pamoja na masuala mbali mbali ya kimaendeleo yaliyoasisiwa na Serikali za CCM kwa awamu tofauti za Uongozi.

Pamoja na hayo aliwapongeza Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum Pemba kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Naye Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl.Queen Mlozi alikemea vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watoto wa Kike vinavyochangia kukwamisha maendeleo ya wanawake katika kunufaika na fursa za elimu.

Mwl.Queen aliwasihi Wazazi,Walezi pamoja viongozi wa dini na kisiasa kusimamia ajenda za kulinda na kutetea haki za wanawake hasa vijana na watoto ili wanufaike na fursa mbali mbali ndani ya jamii.

Akizungumzia changamoto za dawa za kulevya kwa vijana, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania bara Ndugu Jesca Mbogo alisema baadhi ya vijana kisiwani Pemba wameingia katika changamoto za kutumia dawa za kulevya hali ambayo ni hatari katika ustawi wa maendeleo ya nchi.

Mapema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba, ndugu Bimkubwa Khamis Mohamed alisema hali ya kisiasa ndani ya mkoa huo imeendelea kuimarika na wanawake wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiunga na CCM.

Alisema Pemba ya Sasa sio Pemba ya zamani kwani wananchi wengi wameanza kutambua ukweli baada ya kuona kwa vitendo mambo mema yanayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.


Hivyo makala MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA

yaani makala yote MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mwenyekiti-wa-uwt-taifa-bigaudensia.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA"

Post a Comment

Loading...