Loading...
title : KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
link : KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
* Wajadili changamoto na mikakati ya kuimarisha ukombozi wa mwanamke, waiomba Serikali kuendelea kushirikiana nao
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIKA kuelekea siku ya wanawake duniani mtandao wa jinsia nchini (TGNP) kwa kushirikiana na SIDA pamoja na mashirika yanayotetea haki za wanawake umewakutanisha wadau mbalimbali katika kutathimini miaka 25 ya mkutano wa Beijing.
Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza katika mkutano huo uliolenga kujadili mafanikio ya miaka 25 ya mkutano wa Beijing Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema kuwa ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za kimaendeleo bado unahitaji msukumo zaidi ili kuwajenga wanawake katika kujikomboa zaidi.
Akizungumzia kuhusu changamoto Lilian amesema kuwa, vikwazo vimepungua na masuala kama unyanyasaji wa kijinsia, umiliki mali na ushiriki wa wanawake katika shughuli za kimaendeleo unahitaji msukumo zaidi kwa wanawake.
Lilian amesema kuwa ili waweze kufikia malengo hayo ya milenia ni kuendelea kuwainua wanawake katika masuala ya kiuchumi, kifikra na kielimu sambamba na kutoa mawazo na maamuzi katika masuala mbalimbali. Amesema kuwa kupitia mkutano huo wamejadili masuala mbalimbali ya kuweka usawa na kuondoa zile dhana potofu kuhusiana na haki za mwanamke.
Mwanzilishi wa mfuko wa wanawake nchini Mary Lusimbi amesema kuwa mkutano wa Beijing umewafungua wanawake hasa katika kujua haki zao na kutafuta fursa na ameiomba serikali kwenda nao pamoja ili kupata matokeo chanya. Amesema kuwa miongoni mwa mambo waliyojadili na yamefanyiwa kazi kwenye bajeti ni pamoja na suala la usawa wa 50 kwa 50.
Mtandao wa jinsia TGNP umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinaimarika hasa kupitia kampeni mbalimbali ambazo zinapinga ukatili wa ngono na kudumisha haki za watoto.
Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Lilian Liundi akizungumza katika warsha hiyo ambapo amesema kuwa mkutano wa Beijing ulifanyika nchini 1995 ni nguvu na thamani ya mwanamke.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala huo kuelekea siku ya wanawake duniani hapo Machi 8.
Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Lilian Liundi akizungumza katika warsha hiyo ambapo amesema kuwa mkutano wa Beijing ulifanyika nchini 1995 ni nguvu na thamani ya mwanamke.
Hivyo makala KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
yaani makala yote KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kuelekea-siku-ya-wanawake-dunia-tgnp.html
0 Response to "KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO"
Post a Comment