Loading...
title : LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI
link : LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI
LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI
Les Mangelepa ilikuwa ni bensi ya muziki wa dansi iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa dansi maeneo mengi ya Afrika Mashariki na Kati.
Walikuwa wamejikita katika jiji la Nairobi, ambapo waliweza kuwavuta vijana wa wakati huo wakaenda kuserebuka katika kumbi mbalimbali za Nairobi Park, Garden Square, Tents Club na ile ya Park Inn ambako bendi hiyo ilikuwa ikiporomosha burudani.
Baadhi ya vibao murua mbazo zilikuwa mashuhuri na kutamba wakati huo ni pamoja na Embakasi na Nyakokonya.
Les Mangelepa ilikuwa na wanamuziki wengi wakiwa ni raia toka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiwa na makazi yake katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Ilivyoanzishwa bendi hiyo ilikuwa ni mithiri ya msemo wa Waswahili usemavyo kuwa “Kuvuja kwa Pakacha, nafuu kwa mchukuzi” ndivyo ilivyokuwa baada ya bendi ya Baba Gaston kugawanyika.
Baadhi ya wanamuziki wake wakaenda kuunda kikosi cha Les Mangelepa wakiongozwa na Bwammy Walumona ‘La Capitale.’Vijana hao walikuwa nguzo kuu katika bendi hiyo ya Baba Gaston, iliyokuwa ikiongozwa na Baba Nationale Ilunga wa Ilunga.
Yaelezwa kwamba baada ya kuondoka katika bendi hiyo, kulisababisha kifo cha bendi.Bendi Les Mangelepa ilijipatia umaarufu mkubwa kati ya miaka ya 1970na 1980 baada ya kufyatua nyimbo zilizowakuna wapenzi wa muziki wa
dansi katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Baadhi ya nyimbo hizo zilikuwa ni Embakasi, Maindusa, Walter, Safari
ya Mangelepa, Odesia, Dracula, Saad, Maboko Pamba na nyingine nyingi.
Les Mangelepa ilileta ushindani mkubwa katika jiji hilo la Nairobi, dhidi
ya bendi kubwa zilizokuwemo jijini humo.
Baadhi ya bendi hizo ni pamoja na Les Knoirs, Les Wanyika, Orchestra
Shikashika, Orchestra Virunga, Super Mazembe, Baba Gaston na nyingine nyingi.Baada ya ‘kushiba’ umaarufu, pakaingiliwa na mtafaruku mkubwa wa uongozi.Magelepa ikaamua kubadili uongozi, ambapo Kabila Kabanze Eveny, akawa kiongozi wa bendi.
Bendi hiyo ikarejea kwenye umaarufu wake kwa kupiga muziki waKikongo, kama walivyokuwa Super Mazembe na Baba Gaston.Mwaka 1986, Bammy Walumona aliondoka katika bendi hiyo nakuamua kuokoka, lakini aliiacha Mangelepa ikiwa imesheheniwanamuziki wengi wenye vipaji mbalimbali.
Wanamuziki waliokuwa wakiunda kikosi cha Les Mangelepa kiliwajumuisha kina Bwami Walumona ‘Le Capitale’ ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo.Kabila Kabanze ‘Evani’ aliongoza safu ya waimbaji wakati KalengaNzaazi ‘Vivi’, Lutulu Kaniki ‘Macky’ na Babibanga Watshilumba ‘Kai’ walikuwa waimbaji mashuhuri wakati huo. Kai pia alikuwa ni mpuliza
tarumbeta na trombone.
Kwenye drums na gitaa la besi alipiga Kasongo Fundi Petit Jean, Lukangika Maindusa ‘Moustano’ alikuwa akipiga gitaa la solo na rhythm
wakati Mwepe Mutshi ‘Cavalou’ naye alisimama kwenye upulizaji wa tarumbeta.Mwanamuziki mwingine alikuwa Lumwanga Mayombo ‘Ambassador’
aliyekuwa akiliungurumisha gitaa zito labesi na rhythm.
Drums ziligongwa na Mukala wa Mulumba ‘Bebe’, naye Tabu Ngongo Ildephonce ‘Super Sax’ na Tshimanga Zadios walikuwa wakipuliza
saxophone.Kundi hilo machachari pia lilikuwa na wanamuziki wengine kina Twikalewa Twikale na Kabe Kimambe ‘Elombe’ walikuwa wakibofya kinanda nakupiga gitaa la solo. Kabebe Mukangwa ‘Picolo’ na Tambwe Lokasa
walikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi.
Tumba ziligongwa na Mukala Kanyinda ‘Coco’ ambaye alikuwa na
uwezo wa kupuliza hata saxophone.Mwanamuziki mwingine alikuwani Padd ‘Ma Wauwau’ aliyekuwaakipuliza saxophone.Tungo za nyimbo za Mangelepa zilishika chati katika miji mingi hapanchini hususan kwenye kumbi za burudani na maeneo ya starehe namabaa.Wimbo wa ‘Embakasi’ na ‘Kanemo’ zilitungwa na mwanamuziki
Kalenga Nzaazi ‘Vivi’, hadi leo ukipigwa popote watu wengi hufuatilia
neno kwa neno.Nyimbo za ‘Mimba’ na ‘Nyako Konya’ zilitungwa na mwanamuzikiBadi wa Tshilumba nazo zinaendelea kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki hadi leo.
Wimbo wa ‘Maindusa’ ulioimbwa na kupigwa kwa umahiri mkubwa ni utunzi wake Lukangila Maindusa, wakati wimbo wa ‘Mimba’ na ‘Malawi’ zilitungwa na mwanamuziki Kabila Kabanze ‘Evani’. Wimbo ambao huanza kwa sauti ya juu sana wa ‘Walter’ ni utunzi wake Badi Banga wa Tshilumba. Les Mangelepa baadae wakafyatua albamu nyingine
yenye nembo ya Madima ikiwa imesheheni nyimbo za ‘Madina’,
‘N’kimba’, ‘Lolo Mukena’ na ‘Kawala’.
Bendi hiyo Les Mangelepa itakumbukwa na wapenzi wa muziki wa nchini Zambiaambako ilifanya ziara na kutoa burudani ikiwa humo. Baada ya kurejeawakatoka na vibao vikali vya ‘Dajala’, ‘Saad’, ‘Tshibola’, ‘Mankwazi’ na‘Safari ya Zambia’ wimbo ambao ulipigwa kwa ala tupu.
Mwaka 1978, Mangelepa ambayo ilikuwa ikitumia mtindo wa ‘Chafua Chafua’, walirekodi nyimbo zilizokuwa na sehemu ya kwanza na ya pili za ‘Pambana pambana’ pamoja na ‘Haleluye’. Nyingine zilikuwa ni ‘Dracula’, ‘Mangelepa Kamili’, ‘Kizunguzungu’, ‘Suzanne’ na ‘Trouble’.
Wanamuziki hao walitunga na kuimba nyimbo nyingi zilizokuwa kivutio
cha mashabiki na wapenzi wa muziki. Bendi hiyo ilikuja onekana kama haina mpinzanimiongoni wa bendi zilizokuwa zikipiga katika jiji hilo.
Mangelepa ilijipatia umaarufu mkubwa kati ya miaka ya 1970/80 baada ya kufyatua nyimbo zilizowakuna wapenzi wa muziki katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Nyimbo hizo zilikuwa za ‘Embakasi’, ‘Maindusa’, ‘Walter’, ‘Safari ya Mangelepa’, ‘Odesia’, ‘Dracula’ na ‘Maboko Pamba’.
Mangelepa ikatokea kuwa maarufu kwa miziki wa Lingala kama walivyokuwa Super Mazembe, Baba Gaston na Virunga ya Samba Mapangala.
Mwaka 1986, Bammy Walumona aliondoka katika bendi hiyo, akaamua kuokoka. Licha ya kuondoka kwake bendi hiyo bado ilikuwa imesheheni wanamuziki wengi wenye vipaji mbalimbali.
Waliweza kutunga na kuimba nyimbo nyingi zilizokuwa kivutio cha mashabiki na wapenzi wa muziki Afrika Mashariki na Kenya na kuwa bendi pinzani zilizokuwa zikipiga katika jiji hilo.
Safu ya wanamuziki waliokuwa wakiunda kikosi cha Mangelepa kilikuwa kwa kuanzia upande wa mpigaji wa gitaa lililoongoza la solo, alikuwepo mzee mzima, Bwamy Walumona ‘Le Capitaine’ ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa bendi hiyo.
Kabila Kabanze ‘Evani’ aliongoza safu ya waimbaji wakati Kalenga Nzaazi ‘Vivi,’ Lutulu Kaniki ‘Macky’ na Babibanga Watshilumba ‘Kai’ walikuwa waimbaji mashuhuri wakati huo. Kai pia alikuwa ni mpuliza tarumbeta na turombone.
Kwenye drums na gitaa la besi alipiga Kasongo Fundi ‘Petit Jean’, Lukangika Maindusa ‘Moustano’ alikuwa akipiga gitaa la solo na rhythm wakati Mwepe Mutshi ‘Cavalou’ naye alisimama kwenye tarumbeta.
Mwanamuziki mwingine alikuwa Lumwanga Maoyombo ‘Ambassador’ aliyekuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na rhythm. Drums ziligongwa na Mukala wa Mulumba ‘Bebe’, naye Tabu Ngongo Ildephonce ‘Super Sax’ na Tshimanga Zadios walikuwa wakipuliza saxophone.
Kundi hilo machachari pia lilikuwa na wanamuziki wengine kina Twikale wa Twikale na Kabe Kimambe ‘Elombe’ walikuwa wakibofya kinanda na kupiga gitaa la solo. Kabebe Mukangwa ‘Picolo’ na Tambwe Lokasa walikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi.
Tumba ziligongwa na Mukala Kanyinda ‘Coco’ ambaye alikuwa na uwezo wa kupuliza hata saxophone.
Mwanamuziki mwingine alikuwa Padd ‘Ma Wauwau’ aliyekuwa akipuliza saxophone.
Tungo za nyimbo za Mangelepa zilishika chati katika miji mingi hapa nchini hususan kwenye kumbi za burudani na maeneo ya starehe na kwenye baadhi ya baa.
Bendi hiyo itakumbukwa na wapenzi wa muziki wa nchini Zambia ambako ilifanya ziara ikitoa burudani ikiwa humo na baada ya kurejea wakatoka na vibao vikali vya ‘Dajala’, ‘Tshibola’, ‘Mankwazi’ na ‘Safari ya Zambia’ wimbo ambao ulipigwa kwa ala tupu.
Mwaka 1978, Mangelepa walirekodi nyimbo zilizokuwa na sehemu ya kwanza na ya pili za ‘Walter’, ‘Pambana pambana’, ‘Maboko Pamba’ pamoja na ‘Haleluye’. Nyingine zilikuwa ni ‘Dracula’, ‘Mangelepa Kamili’, ‘Kizunguzungu’, ‘Suzanne’ na ‘Trouble’.
Les Mangelepa haipo tena katika ulimwengu wa muziki na baadhi ya wanamuziki wake wametangulia mbele ya haki, wengine wameokoka na kuacha kabisa kupiga muziki wa kidunia
Mwisho.
Mwandishi wa makala hii aanapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200, 0713331200 na 0736331200.
Hivyo makala LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI
yaani makala yote LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/les-mangelepa-ilivyo-acha-historia.html
0 Response to "LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI"
Post a Comment