Loading...
title : MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE
link : MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE
MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE
*Wapo waliamua kushika gari iliyobeba mwili wake
*...Kwe heri Ruge...nenda kaka,...mbela yako, nyuma yetu
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
Ukweli ni kwamba mwili wa Ruge kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameupokea kwa heshima kubwa na hiyo inaonesha namna alivyokuwa kwenye mioyo ya watu.
Mwili wa Ruge uliwasili nchini saa tisa Alasiri ukitokea Afrika Kusini ambako kabla ya kuanza safari ukiwa uwanjani hapo uliwekwa kwenye gari ndogo yenye rangi nyeusi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dar es Salaam mamia ya wananchi walianza kujipanga kuanzia uwanjani hapo.Aliyeongoza mapokezi ya mwili wa Ruge ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais-Muungano na Mazingira.
Mwili wa marehemu Ruge baada ya kutoka Uwanja wa Ndege ulipita Barabara ya Uhuru, Karume ,Magomeni ,Morocco Hotel,Sinza Kijiweni. Bagama, ITV, Clouds ,Kawe na kisha Lugalo.
Michuzi Blog na Michuzi TV waliokuwa kwenye msafara huo walishuhudia mamia ya watu wakiwa barabarani wakisuburi kuona jeneza lililobeba mwili wa Ruge.
Baadhi ya watu walishindwa kujizuia kiasi cha baadhi yao kuamua kwenda kushika gari iliyobeba mwili wa marehemu Ruge ambaye hakika amethibitisha kuwa alikuwa yupo kwenye mioyo ya Watanzania.
Kutokana na idadi kubwa ya watu iliyojitokeza barabarani, ilisababisha msafara huo kusimama mara kwa mara.Waendesha bodaboda nao walioekana kutokuwa nyuma kwani nao waliamua kuungana na magari yaliyokuwa kwenye msafara huo.
Wakati mwili wa Ruge unapita katika baadhi ya barabara wapo wananchi ambao walikuwa wakisikika wakisema hivi "Nenda Ruge...nenda kaka,...hakika sote ni wa mwenyezi Mungu... nenda Ruge mbele yako , nyuma yetu.
Ukweli ni kwamba kadri msafara wa Ruge ulivyokuwa unaendelea kwenda ndivyo ambavyo idadi ya watu ambavyo ilikuwa inaongeza, kiasi cha cha kufanya gari ambayo imebeba msafara huo kupunguza mwendo na kwenda taratibu.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliamua kutoa maelekezo ya kuhakikisha wananchi waliokuwa barabarani wanapata nafasi ya kuona vizuri jeneza ambalo lilikuwa limebeba mwili huo.
Hata hivyo, aliamua kutoa maagizo ya kuwataka waendesha bodaboda kukaa nyuma ya gari iliyobeba mwili kwani kabla ya kutoa maelekezo hayo , waendesha bodaboda walikuwa wametangalia mbele na kufanya msafara kushindwa kwenda kwa utaratibu mzuri na kutoa nafasi ya wengine kuuona.
Hata hivyo wakati wananchi wengi wakiwa barabarani, kuna wengine ambao wao waliamua kwenda kuusubiri mwili wa Ruge katika Kituo cha Redio cha Clouds.Kwa mujibu wa ratiba mwili wa Ruge kabla ya kwenda Lugalo ulipitishwa katika eneo hilo ambalo ni ofisi zake alizokuwa anafanya kazi enzi za uhai wake.
Sababu za kuupeleka mwili huo Clouds ilikuwa ni kutoa nafasi kwa wafanyakazi wenzake kupata nafasi ya kuona jeneza lililobeba mwili wake.Hata hivyo msafara wa mwili wa Ruge bado unaendelea na Michuzi Blog itaendelea kukufahamisha hatua kwa hatua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na mazingira @jmakamba ameongoza mapokezi ya mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Ruge Mutahaba, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es aalaam Mh.Paul Makonda pamoja na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga.
Mapokezi ya mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Ruge Mutahaba, tayari ukiwa umewasili jioni ya leo.
Hivyo makala MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE
yaani makala yote MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/maelfu-ya-wananchi-dar-wajipanga.html
0 Response to "MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE"
Post a Comment