Loading...
title : Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM
link : Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM
Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Askari Polisi ambao ni wanafunzi katika Chuo cha Taaluma ya Jeshi la Polisi, wakati alipotembelea chuoni hapo kufuatilia maandalizi ya awali baada ya jeshi hilo kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho, kulia ni Mkuu wa Chuo, Naibu Kamishna, Anthony Rutashuburugukwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho,Wengine ni viongozi wa chuo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa ziara katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, jijini Dar es Salaam ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa kutumia wafungwa ili kuweza kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili kati ya Milioni Mia Saba zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli katika Mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Madarasa ya Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea majengo chakavu ya chuo hicho baada ya kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba alizoahidi Rais Dkt. John Magufuli akihutubia katika mahafali ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi chuoni hapo mwishoni mwa mwaka jana
“Wizara ina taasisi ya magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha pesa kuwalipa vibarua wa nje, naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza pamoja na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni vipi mnaokoa kiasi hicho”alisema Masauni
Akitoa taarifa ya awali ya ujenzi huo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Naibu Kamishna Anthony Rutashuburugukwa alitaja majengo yatakayojengwa kuwa ni ghala la chuo, madarasa matatu,bweni moja la askari wa kiume na bweni lingine la askari wa kike.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina wanafunzi wa chuo hicho walimshukuru Rais Dkt. Johh Magufuli kwa kiasi cha fedha alichotoa ili kuweza kujenga sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo mabweni ambayo wamekiri ni chakavu na si rafiki kwa matumizi ya binadamu.
Hivyo makala Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM
yaani makala yote Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/masauni-aokoa-milioni-mia-mbili-za-jpm.html
0 Response to "Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM"
Post a Comment