Loading...

Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini

Loading...
Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini
link : Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini

soma pia


Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi ameiomba Serikali ya Uarabuni kundelea kutoa misaada mbalimbali ukiwamo wa kujenga hospitali kubwa nchini ili kuwasaidia wagonjwa mbalimbali nchini. 
Kauli hiyo imetolewa na Prof. Kambi wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yalioandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Al balsam Cure and Care International Charity Organization kwa ajili ya kuwawezesha wataalam wa afya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa waliolazwa ICU.
“Natambua kwamba Serikali ya Uarabuni imekuwa ikitoa misaada mingi ya kuboresha huduma za afya, hivyo naomba wajenge hospitali kubwa nchini kwa ajili ya kutoa huduma za afya nchini,” amesema Prof. Kambi.
Prof. Kambi amewataka wataalam wanaopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri katika sehemu za kazi pamoja na kuwaelimisha wataalam wengine.
Pia, Mganga mkuu ameishukuru Serikali ya Uarabuni kwa msaada wa matibabu ambao wamekuwa wakitoa kwa hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Muhimbili na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Naye Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa MNH imepanua huhuduma za vyumba vya kulaza wagongonjwa wanaohitaji uangalizi maalamu pamoja na kununua vifaatiba.
Leo, watalaam walikuwa wakifundishwa jinsi vifaa tiba vya ICU vinavyopunguza maumivu kwa mgonjwa na jinsi kudhibiti hewa wakati mgonjwa akipatiwa matibabu ICU. Mafunzo hayo yanawashirikisha wataalam kutoka Hospitali ya Muhimbili, Mbeya, Hospitali ya Benjamini Mkapa, Bugando, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi akizungumza kwenye mafunzo ya  kuwawezesha wataalam wa afya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa waliolazwa ICU. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi wakati akifungua mafunzo hayo.
 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani akizungumza leo kwenye mkutano huo. Bw. Makani alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homoni katika hospitali hiyo, Dkt. Faraja Chiwanga akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo kwa wataalam wa ICU nchini.
 
Wataalam kutoka Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Benjamini Dodoma, Mbeya na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mafunzo hayo
 Bw. Alaa Almqatieb akitoa mafunzo kwa  wataalam mbalimbali wa hapa nchini wakiwemo washiriki kutoka Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Benjamini Dodoma, Mbeya na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa afya pamoja wataalam wengine.


Hivyo makala Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini

yaani makala yote Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mganga-mkuu-ashauri-kujengwa-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini"

Post a Comment

Loading...