Loading...
title : MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE
link : MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE
MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MDHAMINI wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, Robert Katula ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujitoa kumdhamini mshtakiwa huyo kwa kuwa hana ushirikiano.
Lissu anakabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani hapo pamoja na wenzake watatu wakiwemo wahariri wa gazeti la Mawio.
Katula ametoa maombi hayo leo Jumatatu Machi 25, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na mahakama kutaka maelezo ya mdhamini huyo kuhusu hali ya mshtakiwa Lissu.
Amedai, hana la kusema kwa kuwa hajapata taarifa zake na hana mawasiliano wala ushirikiano wowote na mbunge huyo hivyo ikiwezekana ajitoe tu. Hata hivyo, baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba amemwambia kuwa hawezi kujitoa kwa sababu mshtakiwa wake hayupo mahakamani kwa sasa na mahakama aina taarifa yoyote juu yake.
Amesema, kweli rekodi ya mahakama ipo kimya juu mshtakiwa Lissu hivyo ni jukumu la mdhamini kuwasilisha taarifa Mahakamani zitakazoeleza mahali alipo mshtakiwa.
Kufuatia hayo, Mahakama imewapa tena muuda wadhamini kuweza kuwasilisha taarifa za mahali alipo mshtakiwa huyo, "niwaeleze tu kwamba hakuna namna ya nyie kujitoa kama mshtakiwa huyu hatofika mahakamani, mkijitoa nyie nani atakuwa na jukumu la kumleta hapa, " aliwahoji wadhamini wa Lissu.
Naye mdhamini mwingine wa Lissu, Ibrahim Ahmed amedai kuwa wamefanya juhudi za kila aina kupata namba za simu ili kuweza kuwasiliana na Lissu awaeleze mahali alipo na maendeleo ya afya yake lakini imeshindikana.
Kufuatia Maelezo hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 25, mwaka huu.
Kesi hiyo ilikuwa katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka, lakini inashindwa kuendelea kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, ( Lissu )kuwa nchini Ubeljiji kwa ajili ya matibabu.
Lissu na wenzake watatu katika mahakama hiyo wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi katika gazeti la Mawio kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uchochezi ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Hivyo makala MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE
yaani makala yote MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mdhamini-wa-tundu-lissu-aomba-kujitoa.html
0 Response to "MDHAMINI WA TUNDU LISSU AOMBA KUJITOA KWENYE KESI YAKE"
Post a Comment