Loading...

MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU

Loading...
MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU
link : MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU

soma pia


MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa tatu kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara wakielekea kwenye eneo la uchimbaji wa TSF kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akionyesha kwa kuuliza mwisho wa mpaka wa eneo la ujenzi wa TSF mpya, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya Tarime.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekiiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wa kwanza kushoto akitoa taarifa fupi ya hali ya mkoa wake wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tarime.


…………………..


Na Issa Mtuwa – Tarime

Serikali imesema itaufunga mgodi wa North Mara ifikapo Machi 30, 2019 endapo mgodi huo utashindwa kuyadhibiti maji yenye sumu yanayo tiririka kutoka kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji (topesumu) (Tailings Storage Facility -TSF). ya mgodi huo kuelekea kwenye makazi ya watu.

Hayo yamesemwa leo machi 5, 2019 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko alipotembelea mgodini hapo kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mabwawa wa topesumu (TSF) na kuzungumza na uongozi wa mgodi na baadae na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyamongo wilaya ya Tarime kuzungumzia hatima ya malipo ya fidia za wananchi waliohamishwa kupisha shuguli za mgodi.


Biteko amesema serikali hairidhishwi na namna mgodi wa North Mara kwa jinsi wanavyo zingatia swala la utunzaji wa maji yenye sumu kwenye (TSF) zao. Amesema serikali inathamini sana maisha ya watu na mtu mmoja mmoja, na kwamba maisha ya mtu mmoja ni bora kuliko shuguli zote za mgodi.

“ Naomba niseme ukweli, tena kutoka moyoni, sijaridhishwa na hili jambo la utiririshaji wa maji yenye sumu kuelekea kwenye makazi ya watu. Serikali hii ya awamu ya tano ya Dkt. John Pombe Magufuli inathamini sana maisha ya watu wake kuliko kitu chochote. Thamani yamaisha ya mtanzania mmoja ni bora kuliko kinachochibwa hapa. Nitoe rai kwa mgodi ifikapo Machi 30, mwaka huu, hili jambo liwe limekwisha, kinyume cha hapo, nitafunga mgodi mpaka pale mtakapo tekeleza jambo hili” alisema Biteko.

Kwa upande wa uongozi wa mgodi umesema, utatekeleza agizo hilo na kwamba juhudi za kudhibiti topesumu kuelekea kwenye makazi ya watu limepewa kipaumbele na kwamba ndani ya muda huo litakuwa limekamilika.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko aliambatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo akiwemo Kamishna wa Madini Mha. David Mlabwa na Afisa Madini mkoa wa Mara Mha. Nyaisara Mgaya, wengine ni kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa mara wakiongwa na mwenyekiti wake ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Mara bwana Adam Kigoma Malima.

Ziara hiyo inafuatia vikao mbalimbali vya awali vilivyofanyika mwaka huu vikilenga masuala mbalimbali yanoyo husu mgodi huo likiwemo swala la udhibiti wa maji yenye sumu (topesumu) yanayo lalamikiwa na wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi huo, kikao cha kwanza kilifanyika Januari 19, chini ya makatibu wakuu wa wizara saba ((Madini, Makamu wa Rais Mazingira (NEMC), Ardhi, TAMISEMI, Afya, Fedha na Maji)) ambapo serikali ilitoa miezi nane kutekeleza maagizo yaliyopewa.


Hivyo makala MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU

yaani makala yote MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mgodi-wa-norh-mara-kufungwa-iwapo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MGODI WA NORH MARA KUFUNGWA IWAPO HAUTACHUKUA HATUA KUDHIBITI MAJI SUMU"

Post a Comment

Loading...