Loading...
title : MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII
link : MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII
MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Mukune amesaini mkataba
wa kuwa Balozi wa Bodi ya Utalii Tanzania leo March28 2019 kwa kutangaza Utalii wa ndani na kutoa hamasa kwa watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo wa mwaka mmoja Queen Elizabeth anasema kuwa yeye anaona fahari kubwa kupata nafasi ya kuwa balozi wa kutangaza vivutio vyetu hivyo amefurahi kupata nafasi hiyo.
"nimefurahi kupata nafasi ya kutangaza vivutio vyetu ndani na nje ya nchi na naahidi kuitumia nafasi hii vizuri kabisa kwa kutumia nafasi na umaharufu wangu nilionao kwa sasa kwa kuwa mfano wa Mrembo ambaye nitafanya ziara ya utalii wa ndani kama taji langu linavyojieleza kwani nitatoa hamasa kupitia mitandao yangu ya kijamii na makundi yote yanayoniunga mkono hili waweze kutembelea vivutio vyetu vilivyopo hapa nchini"anasema
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa bodi ya Utalii nchini Devotha Mdachi anasema katika kuendelea kutangaza utalii wa nchi wamehamua kutumia vijana wenye ushawishi ili kuzidi kuitangaza utalii wetu kwa watanzania na wageni wanaotuzunguka.
"Tumeamua kumtumia Miss Tanzania kwanza ni kijana pia anaushawishi mkubwa kwa jamii kwa watu wengi kwani ameweza kutuwakilisha kimataifa hivyo kupitia yeye tutaweza kutangaza vivutio vyetu vikafika mbali na kuwafikia vijana wengi hapa nchini ambao wamekuwa wakifatilia masuala ya burudani na urembo"anasema.
anasema wataendelea kuwatumia vijana maarufu kuzidi kutangaza utalii wa nchi na wameshaanza mazungumzo na baadhi yao.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi akizungumza na Waandishi wa habari Kabla ya kutiliana Saini na Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune katika Ofisi za TTB Zilizopo Jijini Dar es Salaam.Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kutiliana Saini Mkataba wa kuwa Balozi wa Bodi ya Utalii Nchini.
Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi wakitiliana saini Mkataba wa mrebo huyo kuwa balozi wa utalii nchini
Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi, Wakibadilishana Mkataba mara baada ya kuliana Saini
Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika kushuhudia utiliaji saini Mkataba wa Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi
Hivyo makala MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII
yaani makala yote MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/miss-tanzania-queen-elizabeth-asaini.html
0 Response to "MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII"
Post a Comment