Loading...

NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA

Loading...
NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA
link : NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA

soma pia


NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA


*Ni yule aliyezungumzwa na Rais Magufuli jana 
Ikulu kuwa amechukua fedha za wenzake bilioni 1.4 

*Aliwaambia anavyoviwanja...wakampa fedha 
akawaliza na kisha kuanza kuwazugusha 

 Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kuwa itamfikisha  Mahakamani leo Mkurugenzi wa Mipango ,Ufuatiliaji na Tathimini wa taasisi hiyo Kulthum Ahmed Mansoor kwa kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu Sh.Bilioni 1.6.

Inaelezwa kuwa Kulthum anadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali na kujipatia fedha taslimu Sh.bilioni 1.4 kutoka kwa watumishi wa TAKUKURU kwa ahadi  ya kuwauzia viwanja vilivyoko katika eneo alilodai alikuwa analimiki kihalali huko maeneo ya Nzole -Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Machi 29,2019 jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi a TAKUKURU Brigedia Generali John Mbungo amesema mtumishi huo alijiunga na taasisi hiyo kama Mkurugenzi wa Mipango,Ufuatiliaji na Tathmini Oktoba 2009 akiwa amehamishiwa kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria.

Kuhusu tuhuma zinazomkabili Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU amesema mwaka 2012 mtuhumiwa huyo akiwa mwajiri wa taasisi hiyo kwa cheo chake aliwajulisha watumishi wa wenzake kwamba analo eneo kubwa la ardhi analolimiliki kihalali katika eneo la Bagamoyo na anataka kuwauzia viwanja watumishi kwa utaratibu wa kulipa fedha taslimu au kidogo kidogo.

Amesema viwanja hivyo ambavyo vilikuwa vya ukubwa tofauti vilikuwa vikiuzwa kwa thamani ya kati ya Sh.5000,000 na Sh.7000,000 kwa mtumishi binafsi kwa utaratibu wa kulipia fedha kidogokidogo au zote.

"Watumishu walikubali na utaratibu huo na walijiorodhesha kununua viwanja hivyo, wao pamoja na ndugu zao na kumlipa Kulthum fedha taslimu au kwa awamu kwa utaratibu waliokubaliana.

" Baada ya makubaliano hayo watumishi waliokamilisha malipo yao walianza kuona dalili za kudanganywa baada ya kutokabidhiwa hati ya kiwanja wala nyaraka yoyote inayoonesha umiliki halali wa kiwanja alichonunua na walipomuuliza alisema viwanja hivyo vina mgogoro anvao uko mahakamani,"amesema.

Ameongeza baada ya kupokea malalamiko ya watumishi dhidi ya Kulthum uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU pamoja na mambo mengine umebaini viwanja vilivyoahidiwa kuuzwa vilikuwa ni zaidi ya 300, fedha alizokwishachukua mtuhumiwa kutoka kwa watumishi kulipia viwanja hivyo zaidi ya Sh.bilioni 1.4

Uchunguzi pia umebaini mtuhumiwa alijipatia fedha nyingine zaidi ya Sh.milioni 200 ambazo alilipwa na watumishi kama gharama kwa ajili ya kulipia hati na nyaraka nyingine za umiliki."Uchunguzi umebaini fedha hizo hazikuwahi kuwasilishwa wizara ya ardhi.Viwanja vilivyokuwa vikizungumzwa kama vinauzwa uchunguzi umebaini Kulthum hakuwa na umiliki wowote zaidi ya kuwa na nyaraka za kughushi.
yafuatayo chunguzi."

Kutokana na uchunguzi huo TAKUKURU iliamua kuchukua hatua ya kumsimamisha kazi mtuhumiwa tangu Machi 8,2018 na kwamba tasisi hiyo inatarajia kumfikisha mahakamani leo kwa makosa ya kughushi ,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na utakatishaji fedha.


Hivyo makala NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA

yaani makala yote NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/news-alert-takukuru-kumfikisha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA"

Post a Comment

Loading...