Loading...

PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA

Loading...
PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA
link : PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA

soma pia


PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema kuwa imeridhishwa na mtambo wa TTMS wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) unavyofanya kazi katika katika kulinda usalama wa Mawasiliano nchini.

Akizungumza wakati Kamati hiyo ilivyotembelea Mamlaka Hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema kuwa wamejiridhisha katika mtambo huo kwa umerahisisha TCRA kufanya kazi kwa ufanisi katika kuweza kusaidia serikali kupata mapato.

Amesema walikuwa na shaka kuhusiana na mtambo huo lakini wamejiridhisha kwa na kuondoa mashaka hayo kwa kamati na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) nao wamejiridhisha na mtambo huo.

Kaboyoka amesema TCRA imepiga hatua nzuri katika mawasiliano kwa kuwa na watendaji mahiri wa kuendesha mtambo huo.

"Uzuri wa mtambo TTMS unasimamiwa na wazawa hii inaoyesha kuwa kila kinachofanyika kitakwenda sawa kuliko mtambo huo ungesimamiwa na watu wa nje"amesema Kaboyoka.Aidha amesema kuwa TCRA iendelee kudhibiti mawasiliano ikiwa ni pamoja na kwenda kukuza uchumi wa nchi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema kuwa mtambo huo unaweza kukokotoa takwimu zote miamala ya fedha unavyofanywa na kampuni za simu kutoka na moja kwenda Mtandao mwingine.Amesema kazi nyingine ni kusimamia simu ndani na nje sambasamba na kutambua simu za ulaghai, uhakiki wa mapato na ubora wa mawasiliano.

Amesema kuanza kwa mfumo huo umesaidia kupunguza simu za ulaghai kutoka asilimia 65 hadi kufikia asilimia 10 ikiwa ni pamoja kuongeza pato la Taifa kwa asilimia 9.8.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Mamlaka hiyo.
 Afisa wa Makumbusho wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Abdulrahman Milasi akitoa maelezo wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo katika Makumbusho ya vitu vilivyotumika zamani katika mawasiliano.
 Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA Dkt Jonas Kilimbe akitoa maelezo kuhusiana na utendaji wa TCRA wakati Kamati ya PAC Ilipotembelea Mamlaka hiyo.
 Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)Jumanne Ikuja akitoa maelezo katika gari la kuangalia masafa wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC)  Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA).


Hivyo makala PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA

yaani makala yote PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/pac-yajiridhisha-mtambo-wa-ttms-wa-tcra.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA"

Post a Comment

Loading...