Loading...

Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki

Loading...
Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki
link : Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki

soma pia


Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki

TIMU ya Taifa ya walemavu wa akili, wanatarajia kuwasili nchini leo mchana ikiwa na medali 15 kutoka katika michezo ya Dunia ya walemavu wa akili iliyomalizika Falme za Kiarabu (UAE).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays katika medali hizo, 12 za dhahabu, fedha moja na Shaba 2 zilizopatikana katika Riadha na Mpira wa Wavu.

Rays alisema michezo hiyo iliyochezwa UEA, michezo ya Riadha ilichezwa Abu Dhabi huku Mpira wa Wavu michezo hiyo ilifanyika Dubai.

Katika mpira wa Kikapu, Tanzania imeibuka mabingwa baada ya kuiadhibu Italia kwa seti 2-1 katika fainali.

Rays alisema katika riadha Tanzania imezoa medali 9 za dhahabu , Fedha moja na shaba 2 ambako Boniventura Anga wa Mtwara alipata medali ya dhahabu.

Aidha katika michezo hiyo, Tanzania ilishiriki michezo hiyo sambamba na wachezaji kutoka kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nyarugusu.

Katika mapokezi hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge anatarajia kuwapokea wanamichezo hao ambao wameiletea heshima Tanzania katika michezo hiyo.

Michezo ya dunia ya majira ya kiangazi yalianza Machi 14 na kumalizika Machi 21 (UAE).


  Mwanariadha Boniventura Anga kutoka Mtwara akionesha medali yake ya dhahabu baada ya kufanya vizuri katika michezo ya dunia iliyomalizika Falme za Kiarabu.
 Picha ya pamoja
 Mkurugenzi wa Special Olympics International (SOI), Tim Shriver akipunga mikono juu na timu ya Taifa ya Tanzania katika michezo ya dunia nchini UAE





Hivyo makala Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki

yaani makala yote Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/special-olympics-kuwasili-nchini-leo-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki"

Post a Comment

Loading...