Loading...

PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER

Loading...
PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER
link : PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER

soma pia


PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Afrika Matters Limited Lyinda Chalker (kulia) jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesema mabadiliko yote ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni katika sekta za madini,maliasili na uwekezaji yana lengo la kuweka mazingira bora zaidi yatakayoleta tija kwa Taifa na wawekezaji kutokana na sheria mpya kuondoa utaifishaji (nationalization) na upokonyaji mali (confiscation).

Profesa Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Mhe. Lynda Chalker na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuweka uwanda sawa kwa kuondoa rushwa na urasimu na kumtaka Mhe Chalker kuhamasisha wawekezaji kutoka Uingereza kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo Profesa Palamagamba John Kabudi amemuahakikishia Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Africa Matters limited kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni salama na yameboreshwa zaidi na hakuna masuala ya utaifishaji (nationalisation) wala upokonyaji mali (confiscation) kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.

“Katika kutekeleza diplomasia ya Uchumi Tanzania inatoa kipaumbele kwa uwekezaji wenye tija kwa Taifa na unaozingatia maslahi ya pande zote (Win – win situation) kwa kuwa sasa kupitia sheria mpya tuna mfumo wa kodi unaofahamika, misamaha ya kodi isiyo na upendeleo na si kweli kuwa mazingira yamebadilika na kusema kweli kilichbadilika ni usimamizi madhubuti,kupambana na rushwa na kuhakikisha kodi stahiki inalipwa”

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Mhe. Lynda Chalker amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuongeza kuwa atakaporejea Uingereza msafara wa wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Uingereza na marafiki wa Jumuia ya madola kama Tanzania wanapewa kipaumbele katika uwekezaji na ujenzi wa viwanda.

“Ninadhani wawekezaji hasa wa nje ya Tanzania wanahitaji kufanya utafiti kidogo kuhusu kile Tanzania inachokihitaji na namna watakavyonufaika kwa kuwekeza Tanzania,nimuahidi waziri hapa kuwa nitakaporejea London, nitakutana na mjumbe maalum wa Uingereza wa mambo ya biashara kwa Tanzania pia nitaonana na mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza na Jumuia ya Madola kuona uwezekano wa kuwa na mkutano mkubwa ambao utazungumzia zaidi masuala ya uwekezaji na biashara kwa Tanzania”


Hivyo makala PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER

yaani makala yote PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/prof-kabudi-akutana-baroness-lynda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER"

Post a Comment

Loading...