Loading...
title : RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO
link : RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO
RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO
*Akumbuka mtekwaji alivyokunywa chai na Mambosasa
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS Dk.John Magufuli amesema anashangazwa na ukimya wa Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na utekaji wa mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewj 'MO'.
Hayo ameyasema leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuapishwa kwa mawaziri wawili baada ya kufanya mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri ambapo Profesa Paramagamba Kabudi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria , amemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wakati Dk.Agustino Mahiga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amemteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Rais Magufuli akiwa anazungumzia utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini ametumia nafasi hiyo kutolea mfano tukio la kutekwa kwa MO ambaye baada ya kutekwa kuna mambo mengi yamezungumzwa.
"Baada ya tukio la kutekwa kwa Mohamed stori zilikuwa nyingi sana, tukaambiwa kuwa kuna wazungu wamehusika.Tukaambiwa ameonekana Gymkhana , watu wanajiuliza aliendaje pale?Aliyeteka akaacha na bunduki , watu wanajiuliza alivyoacha bundiki eneo la tukio je angekutana na wanaomtafuta(Polisi).
"Pia tukaambiwa mtekaji alijaribu kuchoma gari.Baadae tunaona mtekwaji anakunywa chai na Mambosasa. Lazima hili jambo lifike mwisho,watanzania walitarajia mmiliki wa nyumba anakamatwa na Polisi ili ajibu watu waliingiaje nyumbani kwake na wakaa siku zote hizo?
"Watanzania hata kama watakuwa kimya katika jambo hili lakini moyoni wana vingongo sana. Watanzania sio wajinga kwani wanajua kuchambua mambo,"amesema Rais Magufuli.
Wakati anafafanua zaidi kuhusu sakata hilo la MO, Rais Magufuli amesema Watanzania walitarajia kuoana wanaotuhumiwa siku inayofuata wanafikishwa Mahakamani lakini tangu tukio hilo litokee ni miezi sita sasa, hakuna chochote ambacho kimeendelea.
"Watanzania walitarajia kesho yake watuhumiwa wapelekwe mahakamani,basi hata mwenye nyumba alitakiwa kuuliza waliokuwa ndani ya nyumba ni akina nani? Lazima tujenge taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kama lilivyoanzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,"amesema Rais Magufuli.
Akizungumzia zaidi utendaji kazi wa Jeshi la Polisi ,Rais Magufuli amesema wachache ambao wanalichafua Jeshi la Polisi lazima wachukuliwe hatua."IGP wale ambao watashindwa kutekeleza majukumu yako wasiwe wanapelekwa makao makuu bali wawe chini ya Ma-RPC wengine.
"IGP usiogope kuleta majina ya watakaoshindwa kufanya vizuri.Lete tuwatoe nyota zao.Najua wapo ambao wameshindwa kufanya vizuri, ndio maana yule wa Shinyanga tulimtoa kwani katika lile sakata la sukari tunajua nini ambacho kilikifanyika,"amesema Rais Magufuli.
Pia amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu naye hakufanya vizuri, aliyekuwa ana Kaimu Mkoa wa Arusha naye hakuwa anafanya vizuri huku akieleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameponea chupuchupu.
"Amesalimika kwasababu tunajua uwezo wake wa kufanya kazi ni mzuri ndio maana tukaamua kumuangalia na kisha tumempeleka Arusha.Wakati wa tukio la kuibwa kwa Almasi yeye alikwenda kujificha Ukerewe,"amesema Rais Magufuli.
Hivyo makala RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO
yaani makala yote RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/rais-dk-magufuli-ashangazwa-na-ukimya.html
0 Response to "RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO"
Post a Comment