Loading...

RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa.

Loading...
RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa.
link : RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa.

soma pia


RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa.

Andrew Chimesela - Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa na Wilaya ya Kilosa kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuwavamia wananchi wanaolima  katika mashamba yaliyofutiwa umiliki wake na Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Kebwe ametoa kauli hiyo Machi, 3 Mwaka huu alipofanya ziara Wilayani Kilosa iliyolenga kujiridhisha utekelezaji wa mashamba yaliyofutwa mwaka 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na kuagiza mashamba hayo kupangiwa matumizi mengine ikiwa ni pamoja na kuyagawa kwa wananchi wa maeneo jirani na mashamba hayo.
Akiwa Wilayani Kilosa, Dkt. Kebwe aliongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe ambavyo viko jirani na shamba hayo matano kati ya 11 yaliyofutiwa umiliki Wilayani humo huku wananchi waliopewa kuyatumia kwa muda wakilalamika kupewa vitisho na baadhi ya watu kutojihusisha kulima mashamba hayo kwa madai kuwa ni mali yao.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baada ya kupokea malalamiko hayo anaagiza Jeshi la polisi kuwakamata wale wote wanaowatishia wakulima hao. “Na hili naelekeza  Vyombo vya Ulinzi na Usalama, muanze kupekua kuanzia sasa, kama kuna kikundi cha watu kuna watu au hata mtu binafsi kafanya hivyo chukua hatua, kwa sababu sheria zipo” alisema  Dkt. Kebwe. 
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kuwa kila mtu ambaye hana eneo la kulima atapatiwa kupitia mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais ili kila mwananchi aweze kuzalisha na kujikimu kimaisha huku akionya kutoingiza itikadi ya aina yoyote kwenye mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais.

Katika hatua nyingine Dkt. Kebwe amewataka wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe, kufuata utaratibu uliotolewa na Serikali wa kuyatumia mashamba hayo kwa muda wakisubiri mpango rasmi unaoendelea kuandaliwa na Serikali huku akiwaonya wanaotaka kuanzisha mipango mingine ya matumizi ya Ardhi hiyo  kinyume na mipango ya Serikali kusitisha mara moja mipango hiyo.
“Vyombo vyangu vinaniambia wale walikwenda wakavamia maeneo hayo walitaka waanzishe  mpango mwingine mpya, yaani juhudi zote hizi ambazo Serikali imefanya kwake yeye  si kitu. sasa hao mtusaidie tuwafahamu ni akina nani na tuwachukulie hatua, sio kuwafahamu tu” aliongeza Dkt. Kebwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewataka wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kukomesha tabia ya ubishi na ugomvi baina yao, badala yake watekeleze maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuwatahadhalisha kuwa atakayekwenda kinyume na maagizo hayo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za sheria.
Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Kati, Hezekiely Kitilya aliewaeleza wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kuwa Ardhi ya mashamba hayo matano kwa sasa bado ni ya Mhe. Rais na iko chini Kamishna wa Ardhi na wananchi wamepewa kuitumia kwa muda, hivyo ni vema wananchi wakawa watulivu na kuacha ugomvi baina yao.
Sambamba na hilo Bw. Kitilya aliwakumbusha wananchi maelekezo yaliyotolewa na ya Mhe. Rais mara baada ya kuyafuta, ambapo alisema kipaumbele cha kwanza kinawalenga  wananchi wanaozunguka mashamba hayo, cha pili ni kutenga Ardhi hiyo kwa ajili ya Uwekezaji wenye tija wa ndani na nje ya nchi na kuwa na hazina ya Ardhi kwa ajili matumizi mengine ya baadae.
Kwa mujibu wa Afisa Ardhi Wilaya ya Kilosa Bw. Ibrahim Ndembo, alisema Mashamba hayo matano Na. 32 hadi 36 yenye jumla ya Ekari 2,685, baada ya Mhe. Rais kuyafuta, Wilaya ilipeleka maombi Serikalini ili kupewa idhini ya kutumia mashamba hayo kwa muda ombi ambalo lilikubaliwa.
Baada ya kukubaliwana Wilaya iliunda Kamati za ugawaji maeneo ya mashamba hayo na kuyagawa katika sehemu mbili, Ekari 1000 kwa ajili ya wananchi wa Kijiji cha Mvumi na Ekari 1000 nyingine kwa ajili ya kijiji cha Gongwe. Hii inatokana na asili ya vijiji hivyo ambavyo awali kilikuwa ni kijiji kimoja na mwaka 2014 kiligawanyika na kuwa vijiji viwili, Mvumi na Gongwe.
Kwa upande wao Wananchi wa vijiji hivyo akiwemo Bi. Lakero Mkandawile wa kijiji cha Gongwe na Bi. Sara Seleman wa Kijiji cha Mvumi pamoja na Adhi Valaluke wa Kijiji cha Gongwe walimweleza  Mkuu wa Mkoa kero zao kuhusu mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kupewa maeneo ya kulima kwenye mashamba ambayo tayari yana watu, kunyang’anywa mashamba waliokwisha pewa na kutishiwa kukatwa na mapanga tuhuma ambazo zilimhusisha pia Mwenyekiti wa Kijiji cha Mvumi Bw. Abdul Tumbo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe Wilayani Kilosa Mkoani humo kuhusu matumizi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli.
Umati wa Wananchi kutoka Vijiji vya Mvumi na Gongwe waliofika kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuhusu matumizi ya Ardhi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli .
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adamu Mgoyi (anayeongea na kipaza sauti) akiwaonya wananchi kufuata maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusu utaratibu wa kuyatumia mashamba yaliyofutiwa umiliki wake.



Hivyo makala RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa.

yaani makala yote RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/rc-dkt-kebwewanaofanya-vurugu-mashamba.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa."

Post a Comment

Loading...