Loading...
title : TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020
link : TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akifungua mkutano kati ya tume hiyo na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia akitoa utangulizi wa majadiliano katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia kutoka kulia wakiwa pamoja na viongozi wengine wa tume ya uchaguzi katika kutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Picha zikionyesha wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakiwa katika mkutano huo leo.
Tume ya Uchaguzi NEC na Viongozi wa vyama vya siasa wamekutana leo Machi 5,2019 jijini Dar es Salaam ambapo kwa sehemu kubwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku wakitumia mkutano huo kujadili namna ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, pia mchakato wa uchaguzi mkuu ili kuhakikisha unakuwa huru na haki.
Akizungumza mbele ya viongozi wa vyama vya siasa , Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Semistocles Kaijage amesema wadau na watanzania wanafahamu kuwa nchi yetu ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 .
“Katika maandalizi hayo ,Tume chini ya Ibara ya 74(6) ya Katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977 imepewa mamlaka ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ikiwa ni pamoja na jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara,” amesema.
Ameongeza kuwa NEC imeanza maandalizi ya mchakato wa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni mkakati wa kujiandaa na Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2020.
Amefafanua kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ,sura ya 324 na ya kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa sura ya 292 ,Tume inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na uchaguzi mwingine unaofuata.
“Napenda kuwataarifu ,Tume inaendelea na maandalizi ya kuboresha Daftari ambapo mpaka sasa tayari imekamilisha baadhi ya michakato kama vile uhakiki wa vituo vya kujiandikisha ,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji daftari na mkakati wa elimu ya mpiga kura,” amesema Jaji Kaijage.
Ameongeza mchakato wa uhakiki wa vituo lililenga kuona kama kuna haja ya kuongeza vituo katika baadhi ya maeneo, vituo vilivyopo kama bado vinakidhi matakwa ya kisheria na kufanya marekebisho mengine kama kubadilisha majina ya vituo au kurekebisha majina ya vituo yaliyokosekana.
Jaji Kaijage amesema matokeo ya uhakiki huo kwa Tanzania Bara yanaonesha kuwa vituo vya kuandikisha wapiga kura vimeongezeka kutoka vituo 36,549 vilivyotumika kuandikisha wapiga kura mwaka 2015 hadi vituo 37,407.Vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka Kijiji/ Kata mmoja kwenda kata nyingine.
“Matokeo ya uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa Tanzania Zanzibar yanaonesha kuwa vituo vimeongezeka kutoka 380 hadi vituo 407 na kwamba wadau watapewa orodha ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kabla kuanza kwa mchakato wa daftari la kudumu la wapiga kura,” amesema.
Kuhusu vifaa kwa ajili ya uboreshaji wa daftari hilo ,Jaji Kaijage amesema mchakato wa kupata vifaa vya kukarabati mashine za BVR umekamilika na kinachosubiriwa ni kufanyia majaribio ya uandikishaji katika kata mbili za Kihonda iliyopo Manispaa ya Morogoro na Kata ya Kibuta iliyopo wilayani Kisarawe.
Amefafanua ni kawaida kabla ya kuanza kwa mchakato wa uandikishaji ,hufanyika majaribio ili kuona namna na jinsi vifaa vya uandikishaji vinavyofanya kazi katika mazingira tofauti ,lengo likiwa ni kupata na kuwa na namna bora ya kufanikisha mchakato huo.
Ameongeza maandalizi mengine ambayo tayari yamefanyika ni uchapishaji wa miongozo mbalimbali kwa wadau ikiwemo ya kutoa elimu kwa mpiga kura na maelekezo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,kwa watendaji na wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa.
Pamoja na mambo mengine Jaji Kaijage amesema Tume imejiwekea utaratibu wa kuwashirikisha wadau katika hatua mbalimbali za uchaguzi ,kwa lengo la kuhakikisha inajenga na kutekeleza misingi ya kidemokrasia katika kusimamia ,kuratibu na kuendesha chaguzi zilizo huru ,wazi ,za haki na kuaminika.
“Madhumuni ya kukutana kwetu leo ni kuwafahamisha kuwa Tume imekamilisha jukumu lake la kuhuisha na kuboresha kanuni ambazo ziliandaliwa chini ya sharia hizo mbili mwaka 2008.
” Tume imeona ni vema ikawapitisha katika kanuni hizo kwa kuangalia Yale maeneo ambayo yamefanyiwa marekebisho ama kwa kuondoa au kuongeza vifungu lakini kwa kueleza sababu za marakebisho hayo,”amesema Jaji Kaijage.
Hivyo makala TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020
yaani makala yote TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/tume-ya-taifa-ya-uchaguzi-yakutana-na.html
0 Response to "TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA, LENGO NI KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020"
Post a Comment