Loading...
title : SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI
link : SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI
SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii
WATU saba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la tuhuma za wizi wa mapipa 20 ya mabaki ya madini yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 900.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Mbando, Wakili wa Serikali Jenifa Masue amewataja washtakiwa hao ni Jacob Kihombo, Yahaya Masoud, Mbaraka Lipinda, Ramadhani Zombe, Waziri Kibua, Mustapha Mnyika na Richard Sàngana.
Imedaiwa kati Februari 6 na 7 mwaka huu ndani ni Jiji la Dar es Salaam washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa la kula njama ya wizi wa mali inayosafilishwa.
Katika shitaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa waliiba mali hiyo ambayo ni mapipa 20 ya mabaki ya madini aina ya Tantalite Concentrates yenye thamani ya Sh.938,339,907 mali ya Kampuni ya Bollore Transport and Logistics.
Shitaka la tatu linalomkabili mshtakiwa Zombe peke yake ambaye ni mlinzi, anadaiwa siku hiyo akiwa mwajiriwa wa Kampuni ya Bollore, kama mlinzi, alishindwa kuzuia kutendeka kwa kosa la wizi wa mapipa hayo ya madini.
Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka katika taasisi zinazotambulika na serikali watakaosaini bondi ya Sh. milioni 52 kila mmoja.
Pia mdhamini au mshitakiwa ametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya milioni 52. Kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Hivyo makala SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI
yaani makala yote SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/saba-kortini-kwa-tuhuma-za-wizi-wa.html
0 Response to "SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI"
Post a Comment