Loading...

KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA

Loading...
KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA
link : KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA

soma pia


KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA

*Ni baada ya mashahidi kukosa nauli ya kuwafikisha mahakamani 

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

KWA mara nyingine tena, kesi ya kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake imekwama kuendelea kusikilizwa kwa kuwa mahakama haina fedha ya kuita mashahidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa amedai leo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa wameshindwa kuita mashahidi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu hawana fedha za kuwalipia nauli.

Mbagwa amedai kesi hiyo ilipangwa leo Machi 26, 2019 kwa ajiri ya kusikilizwa shahidi wa upande wa mashtaka lakini wameshindwa kuwaita mashahidi kwa sababu hawana fedha za kuwalipia nauli. 

"Tumeshindwa kupata mashahidi kwa sababu wote wanatoka nje ya Jiji la Dar es Salaam na wamesema hawana uwezo wa kujisafirisha kuja kutoa ushahidi, " amedai Mbagwa.Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amedai anaomba suala la kuwaita mashahidi lifanyiwe kazi haraka.

Hata hivyo Hakimu Simba amesema, malipo ya mashahidi yana utaratibu wake na kwamba mahakama yake italifanyia kazi na watalitatua suala hilo kwani linazungumzika.Kwa kukumbusha tu ni mara ya pili kwa kesi hiyo imekwama kuendelea kusikilizwa baada ya mwanzoni mwa Oktoba mwaka jana kushindwa kusikilizwa kwa ukosefu wa fedha.

Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 8, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu. Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh.bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.


Hivyo makala KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA

yaani makala yote KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kesi-ya-mhasibu-wa-takukuru-kumiliki.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA"

Post a Comment

Loading...