Loading...
title : Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye
link : Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye
Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Serikali imesema katika sekta ya mawasiliano na kufanya nchi zingine kuiga katika mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA).
Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) amesema katika mawasiliano Tanzania imepiga hatua kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Nchi zilizo kusini Mwa Afrika.
Nditiye amesema kuwa nchi nyingi zinajifunza katika udhibiti wa mawasiliano pamoja na kuangalia gharama za utoaji huduma kwa TCRA katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za mawasiliano.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika mawasiliano kutokana na Teknolojia za mawasiliano hayo kubadilika kila siku.
Aidha amesema mkutano huo watachagua viongozi ambapo na kutoa tathimini ya mawasiliano ambapo Tanzania tuko nafasi nzuri kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema changamoto ya mawasiliano ni watumiaji wenyewe katika vifaa vya mawasiliano.Amesema mtu ananunua simu lakini matumizi yake hajui ambapo anaweza kuminya kitufe chochote bila kujua na mwisho wa siku anatuma vitu vilivyokuwa nje ya maadili ya watanzania.
Mhandisi Kilaba amesema kuwa katika matumizi ya Data Tanzania tuko chini ukilinganisha na nchi nyingine na hiyo ni kutokana na uwekezaji wa miundombinu ya kuwaunganisha watoa huduma.Amesema hata upigaji wa simu kwenda mitandao moja ni ndogo na kufanya kila mtanzania kumudu mawasiliano ya kumiliki simu.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) pamoja na wageni waalikwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jimmy Yonas akitoa maelezo katika mkutano mkuu wa CRASA uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye alizungumza na wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akitoa maelezo kuhusiana na mkutano mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) uliofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa Tanzania ndio wenyeji wa mkutano huo.
Hivyo makala Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye
yaani makala yote Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/serikali-imewekeza-nguvu-katika-sekta.html
0 Response to "Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye"
Post a Comment