Loading...
title : SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA
link : SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA
SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mlango wa matumaini kwa wanawake na Vijana Tanzania DHWYT Clemence Mwombeki akitoa mafunzo kwa Wanafunzi waliohudhulia Mafunzo Juu ya Usawa wa Kijinsia ,Ukatili na Rushwa ya Ngono maeneo ya kazi na Shuleni.
Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wakisikiza Mafunzo kuhusiana na Afya ya Uzazi pamoja na Ujasiliamali katika kuadhimisha siku ya wanawake Dunia Mkoani Mtwara.
Mratibu wa Huduma za Afya ya uzazi Baba,Mama na Mtoto Mkoa wa Mtwara Bi.Rosalia Arope akitoa mafunzo juu ya Afya ya Uzazi kwa wanafunzi wa Vyuo katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mkoa wa Mtwara.
Blandina Emanuel Nguli Mwanafunzi wa Kozi ya sekretari chuo cha Utumishi Mkoani Mtwara akiuliza swali juu ya Afya ya Uzazi katika mafunzo yaliyofanyika siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Shirika la Mlango wa Mtumaini Tanzania.
NA JOSEPH MPANGALA,MTWARA
Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani shirika lisolokuwa la kiserikali la Mlango wa matumaini kwa wanawake na Vijana Tanzania DHWYT limetoa elimu kwa Wanafunzi wa Vyuo kuhusiasna na elimu ya afya ya uzazi pamoja na Ujasiliamali Mkoani Mtwara.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na jinsia zote huku wanafunzi wengi wakitaka kujua juu ya afya ya uzazi baba,mama na Mtoto hasa katika taratibu za upatikanaji wa mimba na umuhimu wa Baba kuhudhulia kliniki pamoja na Athari zake iwapo hata hudhulia.
Akizugumza katika mafunzo hayo Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Baba,Mama na mototo Mkoani Mtwara Bi.Rosalia Arope amesema wanawake wengi wamekuwa wakiwatumia madereva wa Boda boda kama waume zao na kwenda nao Kliniki kwa kuwalipa kiasi kidogo cha pesa kutokana na taratibu zilizowekwa kliniki za kuja na baba wa Mtoto.
“Kuna wanawakewanapokuja Kliniki unabaini kuwa sio mwenza wake halisi anamchukua tu dereva wa bodaboda ili aweze kukidhi kwa sababu kuna baadhi ya wilaya wamejiwekea sheria ndogo kila mwanamke lazima aje na mume wake kwahiyo anaamua kumchukua Dereva Boda boda ili kuepukana na Kero hiyo”amesema Bi.Rosalia.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Mlango wa Matumaini Tanzania amewataka Vijana kushiriki katika maswala mbalimbali ya kijamii kama moja ya njia ya kufatilia maendeleo katika jamii inayowazunguka kuanzia ngazi ya mtaa kata mpaka wilaya.
Hivyo makala SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA
yaani makala yote SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/shirika-la-dhwyt-yatoa-elimu-kwa.html
0 Response to "SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA"
Post a Comment