Loading...
title : StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA
link : StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA
StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA
Siku ya kimataifa ya wanawake duniani husherehekewa kila mwaka inapofika tarehe 8 ya mwezi Machi. Katika kuadhimisha siku hiyo, wafanyakazi wanawake kutoka Kampuni ya Star Media (T) Ltd walitembelea kituo kinacholea watoto wenye uhitaji cha CHAKUWAMA na kukabidhi msaada kwa ajili ya matumizi mbalimbali kituoni hapo.
Miongoni mwa vitu vilivyotolewa na StarTimes ni magodoro ya kulalia, mitungi ya gesi, pampers kwa ajili ya watoto wadogo, mchele, maharage, unga wa mahindi, maziwa ya unga, maji ya kunywa, sharubati, sukari, mafuta ya kupikia, nyanya na vitunguu pamoja na pesa taslim Tsh 450,000 kwa ajili ya kulipia umeme na maji.
“Katika siku hii muhimu ya kuadhimisha wanawake duniani, tuliona ni vyema kushiriki na wenye mahitaji kwa kila tulichojaaliwa tunarudisha kwa jamii hii inayotuzunguka. Tunaamini katika kutoa kwa sababu ndipo ubinadamu ulipo. Tumefarijika sana kuwaona mkiwa na furaha.” Joan Usiri Afisa Rasilimali watu, StarTimes.
Kituo cha CHAKUWAMA kipo jijini Dar es Salaam mtaa wa Sinza na kwa sasa kina jumla ya watoto 68 wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi ishirini.
“Tunawashukuru sana kwa msaada huu mliotuletea lakini zaidi kwa upendo wenu na kukumbuka kuwa kuna jamii ambayo ingeweza kufaidika na mchango wenu. Mungu awabariki sana. Sisi tutaendelea kuwalea katika maadili mema ili badae waje kuwa kama nyinyi na pengine wasaidie watu wengi zaidi.” Bw. Hassan Katibu wa kituo cha CHAKUWAMA.
Afisa Rasilimali watu Kampuni ya StarTimes, Joan Usiri (kulia) akikabidhi msaada kwa Katibu wa kituo cha CHAKUWAMA Hassan
Afisa Rasilimali watu Kampuni ya StarTimes, Joan Usiri (kulia) akikabidhi msaada kwa Katibu wa kituo cha CHAKUWAMA Hassan
Hivyo makala StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA
yaani makala yote StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/startimes-yatoa-msaada-kwa-kituo-cha.html
0 Response to "StarTimes yatoa msaada kwa kituo cha watoto CHAKUWAMA"
Post a Comment