Loading...

TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL

Loading...
TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL
link : TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL

soma pia


TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MACHI 8 ya kila mwaka Tanzania huungana na mataiafa mengine duniani kusherehekea Madhimisho ya Siku ya Wanawake.
Hongereni wanawake wote  Tanzania.Machi 8 ya kila mwaka ni siku muhimu katika maisha yenu.Ndio siku ambayo hutumika kutafakari maisha ya wanawake waliko katika nyanja mbalimbali.Ndio siku ambayo hutumika kuweka mipango na mikakati ya kumkomboa mwanamke.
Ni jambo nzuri, ni jambo lenye tija na kubwa zaidi ni jambo lenye kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume.Siku ya leo hutumika kuangalia haki sawa kati ya wanawake na wanaume.Ndio siku ambayo wanawake hukutana na kufanya mijadala, makongamano na mikutano ambayo kimsingi inaangalia changamoto zinazomzunguka mwanamke na kisha kutafuta ufumbuzi wake.
Ukweli wanaume wamefika mahali wamekubali na kumtambua mwanamke kama kiumbe mwenye thamani kubwa katika maisha ya mwanadamu.Mwanamke kimaumbile ndiye aliyepewa jukumu la kuleta mtanzania mpya duniani.Ndio mama zetu, ndio dada zetu, ndio bibi zetu, ndio shangazi zetu, ndio wake zetu.Hata wifi anapatikana humo humo katika kundi la wanawake.
Kwa kutambua thamani yao , Tanzania kama ambavyo zipo chini nyingine duniani waliamua kutumia Machi 8 ya kila mwaka kama sehemu ya kuadhimisha siku ya Wanawake ambayo huadhimishwa kwa njia mbalimbali lakini msingi mkuu ni kuona wametoka wapi, wako wapi na wanakwenda wapi.
Kwa Ujinga wangu najaribu kuitazama siku hii kwa jicho la aina yake sana.Ndio ambayo wanawake wakiitumia vizuri watatoka na muelekeo ambao utahitimisha kila aina ya unyanyasaji dhidi yao.Wakiitumia siku ya leo itatoa fursa ya kuwa na sauti kwenye jamii inayowazunguka.Wakiitumia vizuri maadhimisho ya siku ya wanawake watakuwa na nafasi pana ya kupigania na kutetea maslahi yao.
Nimeona na kushuhudia taasisi , masharika ,kampuni na maeno mbalimbali wakijadiliana namna ya kumkomboa mwanamke hasa kwa yale mambo ambayo bado wanaona hana nafasi.Ni ukweli usiopingika kuna baadhi ya sheria ambazo zimekuwa changamoto kwa mwanamke.Sheria kandamizi dhidi ya mwanamke zimekuwa zikipigiwa kilele.Ni wakati sahihi wa kuhakikisha yanafayika marekebisho kwa zile sheria ambazo zinalalamikiwa.
Sitaki kuzungumzia Sheria ya Ndoa ambayo nayo kwa muda mrefu inapigiwa kelele.Sitaki kuizungumzia maana mjadala wake ni mpana na unahitaji muda.Ninachotaka kumaanisha bado kuna sheria ambazo zinatumika nchini lakini kiuhalisia si rafiki kwa mwanamke na huenda zikawa chanzo cha kurudisha maendeleo yake nyuma.
Wakati naitafakari Siku ya Wanawake Duniani , ghafla nikaanza kuwaza na ule msemo usemao katika mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke.Sikatai, ndio ukweli.Nipo kwenye jamii hii hii, natambua mchango mwanamke katika kuleta maendeleo kwa ngazi mbalimbali.Ukiona familia imefanikiwa na kupiga hatua ukifuatilia utabaini mchango mkubwa wa mwanamke.Iko hivi mwanamke akiyumba na nyumba lazima itayumba.Akiwa imara na nyumba itakuwa imara.
Hivyo hivyo katika ngazi nyingine za kimaamuzi.Katika maeneo ambayo wanawake wameamianiwa utaona mambo yanavyokwenda vizuri.Kinachonifurahisha mimi wanawake wengi ni waaminifu, wachapakazi na hodari katika kutekeleza majukumu yao.Hivyo wakati mnaitafakari siku ya mwanamke ni vema mkatafakari  namna nzuri ya kuendelea kuunganisha nguvu ambayo mwisho wa siku itamuacha mwanamke akiwa huru kwa kila kitu.
Kwa nchi yetu ya Tanzania, tumepiga hatua kutokana na jitihada ambazo zinaendelea za kuhakikisha mwanamke anakuwa na nafasi sawa na mwanaume.Tunakwenda vizuri na ndio
maana si ajabu kumuona Makamu wa Rais wa Tanzania ni mama .Tena ni mama shupavu na hodari.Huwa namuangalia Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kisha napata somo kubwa kwamba Wanawake wanaweza.Hongereni.
Ushauri wangu, wanawake wakati mkienddelea kudai usawa, ni wakati sahihi pia wa kuangalia kama mwenendo wenu uko sahihi au laa.Naeleza hivyo kwasababu huwa naona kuna baadhi ya maeneo wanawake wanakwamishana wao kwa wao.Huwa natamani kusema adui wa mwanamke ni mwanamke.
Hivyo wakati mnajadili mengi kuhuu mfumo dume na changamoto nyingine, ni wakati sahihi wanawake wakabadilika na kutambua kabla ya kunyoosha vidole wanaume wakajinyooshea na wao wenyewe.Nikiri si wanawake wote lakini kwa sehemu kubwa wamekuwa na tabia ya kupigana vijembe, kuchongeana na baya zaidi hawataki kuona mwanamke mwenzao anafanikiwa.Hili ni tatizo ambalo linahitaji kupata ufumbuzi kwa mustakabali wa mwanamke wa Tanzania.
Yote ambayo nimeandika hapo juu na wewe ukaamua kuyasoma tena kwa hiari yako ni muhimu lakini la kuzingatia zaidi na ambalo limesukuma kuandika maelezo hayo ni maisha ya 'House Girl' (Mfanyakazi wa kike wa ndani ya nyumba). Maisha ya House Girl ambaye kimsingi naye ni mwanamke na leo ni siku yake pia yametawaliwa na changamoto lukuki.Kwa bahati mbaya sana wanaomsemea House Girl ni wachache sana ukilinganisha na changamoto ambazo zimewazunguka.
House girl ni muhimu sana katika maisha ya familia na hiyo ni kutokana na majukumu waliyokabidhiwa na baadhi ya familia.Kuna nyumba ambazo House Girl anakuwa wa kwanza kuamka na mwisho kulala.Familia ya watu sita au nane wote wanamtegemea House Girl ndio afanye kila kitu.Hakuna mwenye kuwaza kumsaidia .Sawa wanawalipwa kwa kazi anayofanya lakini lazima kuangalia aina ya maisha yake.
Ni mwanamke ambaye anahitaji huruma, anahitaji kusaidiwa, anahiti kupata furaha mahali anakoishi.Chakula ambacho familia inakula muandaaji wake ni House Girl,usafi wa nguo, nyumba, watoto , kuteka maji, kusikindikiza watoto shule yote ameachiwa yeye.Hana muda wa kumpumzika na anayesababisha hivyo ni mwanamke mwenzake (Mama Mwenye nyumba).
Nitoe rai ni vema Siku ya Mwanamke ikatoa nafasi ya kujadili maisha ya House Girl.Wengi wao wanateseka na hawana pa kwenda.Kazi kubwa wanayoifanya haiendani na mshahara ambao anautapa kwa mwezi.Akidai kuongezewa mshahara utasikia anaambiwa kwani unakula wapi?
Jamani house girl ni mwanamke na anastahili thamani yake kama mwanamke.Hivyo wakati leo hii wanawake mmeungana kujadili changamoto ambazo mnakabiliana nazo, tumie nafasi hii kujadili namna ya kumuondolea changamoto mfanyakazi wa ndani.
Kutoishi vizuri na mfanyakazi wa ndani madhara yake ni makubwa.Unajua kwanini?Iko hivi
mama unapoamua kumchukia dada wa kazi, kumnyanyasasa, kutomthamini na hata kutomjali yeye anachokifanya anarudisha hasira kwa watoto.Mama ukiondoka kwenda kazini anasema afadhali sasa nami ni zamu yangu kulipiza kisasi.
Tukiishi na house girl vizuri hata familia itakuwa salama.Hivyo leo hii iwe chachu ya kumuondolea changamoto.Ni mwanamke kama walivyo wanawake wengine.Kufanya kazi kwenye nyumba yako si kigezo cha kumuona hana thamani anayostahili kupewa mwanamke.Nimewaza tu kwa Ujinga wangu kama vipi achana nayo.



Hivyo makala TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL

yaani makala yote TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/tukimaliza-siku-ya-mwanamke-tutafakari.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL"

Post a Comment

Loading...