Loading...

Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu

Loading...
Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu
link : Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu

soma pia


Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu

WAFANYAKAZI wanawake wa Benki ya Rasilmali Nchini (TIB) wameazimisha siku ya Wanawake Duniani  kwa kuwakumbuka Wanafunzi wa kike kwenye shule ya Msingi Mbutu , Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao walipofika shuleni hapo wakishirikiana na walimu wa shule hiyo waliwakusanya wanafunzi wa kike kuanzia darasa la tano hadi la saba ili kuzungumza nao. Wakiwaongaza kwa maneno "Mimi ni thamani mimi ni jeshi kubwa."

Mkurugenzi wa Mikopo wa Benk ya TIB Adolphina William akizungumza na Michuzi Blog aliiambia kuwa wamefika shuleni hapo kwa dhamira ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuzungumza na wanafunzi wa kike ambapo walijikita kwenye kuwajengea uwezo, kujitambua , kujithamini kama wanawake.

Adolphina amesema kuwa Benki hiyo inamthamini Mwanamke katika kila nyanja na kwamba leo wameonelea umuhimu wa kuadhimisha siku hii muhimu kwa  kuwaelimisha wasichana ambao ndio wanawake wa baadaye .

"Tumezungumza na wanafunzi hawa wa kike tumewapa elimu ya kujitambua kujithamini na usafi wao".amesema. Amesema kuwa hawakuishia kuwafundisha umuhimu wa usafi kwa kuwapa  Taulo za kike ili ziwasaidie kwenye usafi pia kujijengea mazoea hayo. Benki hiyo yenye Makao Dar es Salaam pia inamatawi Mkoani Arusha, Mbeya  na Mwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Walimu wa shule hiyo Mwalimu Mkuu Msaidizi Venosa Mmassy amefarijika  kuona kuwa taasisi hiyo ya Serikali hasa wanawake wanaofanya kazi kwenye taasisi hiyo kuwakumbuka watoto wa kike na kuamua kuja kujiunga nao kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Amesema licha ya kutoa zawadi lakini wametoa elimu itakayowasaidia wanafunzi hao kwenye maisha yao yote. Naye Lydia Koloseni ameongeza kuwa Wanawake wa Benki ya TIB wamekuwa wazalendo na mifano ya kuigwa kwenye jamii. Mwanafunzi wa Darasa  la saba kwenye shule  hiyo Christina Venance amewashukuru wanawake wa benki hiyo na kwamba wao wamejifunza mengi hasa elimu ya jinsia.
 Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TIB Adolphina William akimkabidhi Mwanafunzi wa Kike ambaye ni mlemavu wa masikio Grace Jonh Taulo za kike  katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani
Picha ya Pamoja kati ya Walimu wa kike wa Shule ya Msingi Mbutu pamoja na wafanyakazi wa Benki ya TIB (katika kuudhimisha siku ya wanawake duniani)
Wafanyakazi wa Benki ya TIB wakigawa Taulo za kike kwa Wanafunzi wa shule ya Msingu Mbutu katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.



Hivyo makala Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu

yaani makala yote Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wanawake-wa-tib-wawafariji-watoto-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wanawake wa TIB wawafariji watoto wa kike shule ya Msingi Mbutu"

Post a Comment

Loading...