Loading...

Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika.

Loading...
Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika.
link : Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika.

soma pia


Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika.

mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi yakitolewa na Umoja wa Ulaya ambayo yanafanyika kwa siku tano kwenye ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha.


Washiriki kutoka nchi za Kenya,Rwanda,Malawi,Zambia na wenyeji Tanzania wakimsikiliza kwa makini mkufunzi Bwana Olydcaegers Greet kwenye mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi kwenye mipaka ya nchi isivyo fuata utaratibu.Mafunzo hayo yametolewa na Umoja wa Ulaya ambayo yanafanyika kwa siku tano kwenye ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha.


Umoja wa Ulaya EU umetoa mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi kwa nchi tano za AFRIKA kwa lengo la kusaidia udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi bila kufuata utaratibu pamoja na utoroshwaji wa vyanzo vya mionzi vilivyoibiwa kwa matumizi yasiyo salaama na hatarishi. 

Washiriki wa mafunzo haya ni kutoka taasisi mbali mbali zikiwemo Mamlaka za Mapato, Forodha na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka katika nchi za Malawi, Rwanda, Kenya, Zambia na wenyeji Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki. 

Huu ni mwendelezo wa mafunzo kwa nchi za Afrika katika kusaidia kupambana na tabia ya uingizwaji wa vyanzo vya mionzi ambavyo kwa namna moja ama nyingine hupelekea kuleta madhara kwa binadamu. 

Mafunzo hayo yanahusisha mafunzo kwa vitendo ikiwemo utambuzi kwa kutumia vifaa maalumu vilivyopo katika mipaka yote katika nchi hizo ambapo husaidia kugundua uhalifu wa namna hiyo. 

Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Tanzania Mhandisi Exavier Zakaria amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia sana hasa kwa wao waliopo katika mipaka amesema wamekuwa wakikutana na masuala mengi ikiwemo baadhi ya wafanyabiashara ambao huenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa za usafrishaji wa vyanzo vya mionzi. 

‘’Ukweli mafunzo yamekuja kwa wakati sahihi na yatasaidia sana katika kuongeza ujuzi kwenye utambuzi wa vyanzo vya mionzi ambavyo ni hatarishi kwa binadamu’’ alisema Mhandisi Zakaria 

Naye mshiriki mwingine wa mafunzo hayo kutoka Tanzania , Bwana Patrick Simpokolwe amesema kuwa kutokana na mbinu za uhalifu za uingizaji wa mionzi isiyo salama katika mipaka mbali mbali katika nchi za Afrika anaamini mafunzo haya yatamsaidia katika kugundua mbinu mbali mbali za uhalifu na kuweza kudhibiti. 

‘’Tumekuwa tukikumbana na udanganyifu mkubwa kwenye mipaka kutokana na mbinu mpya zinazotumiwa na wasafirishaji wa bidhaa mbali mbali zikiwemo zenye vyanzo vya mionzi kutoka na kuingia ndani ya nchi hivyo mafunzo haya yatawezesha kuwabaini wahalifu wa namna hiyo’’ alisema Simpokolwe. 

Mshiriki mwingine kutokea nchini Kenya Bi Evalyne Rotich amesema kuwa kutokana na uwezekanao wa kutokea uhalifu kila wakati na kwamba mafunzo hayo yatawezesha sana kutambua watu ambao sio wema wenye lengo la kupitisha vitu vyenye vyanzo vya mionzi mipakani ambavyo vinaweza kudhuru wananchi katika nchi husika . 

‘’Umakin utaongezeka kwetu kwani mbinu tulizopatiwa zitatuwezesha kutambua vitu vyote ambavyo vitapitishwa bila kufuata utaratibu husika’’ alisema Rotich. 

Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo kutoka umoja wa Ulaya (EU) , Bi Katrijin Vandersteen amesema kuwa katika nchi za Afrika kumekuwa na tatizo la uingizaji wa vyanzo vya mionzi visivyo salama hivyo kwakutolewa mafunzo hayo kutolewa yataweza kusaidia katika uimarishaji wa utambuzi na udhibiti katika maeneo ya mipaka kwenye nchi mbali mbali. 

‘’Tunaamini kuwa washiriki hawa watapata uelewa zaidi juu ya utambuzi wa vyanzo vya mionzi visivyo salama kwa lengo la kusaidia kutoleta madhara kwa binadamu kwenye nchi husika na dunia kwa ujumla mara baada ya kukamilika kwa mafunzo haya ’’ alisema Vandersteen. 

Mfunzo haya yanafanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, jijini Arusha kuanzia tarehe 4 hadi 8 Machi 2019.



Hivyo makala Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika.

yaani makala yote Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/umoja-wa-ulaya-eu-watoa-mafunzo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Umoja wa Ulaya EU watoa mafunzo ya udhibiti wa vyanzo vya mionzi kwa nchi Tano za Afrika."

Post a Comment

Loading...