Loading...

WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO

Loading...
WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO
link : WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO

soma pia


WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO

 Mfanyakazi Mwandamizi ndani ya Ndege (Senior Cabin Crew) Mohamed Ngananya akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusu madai ya Wafanyakazi katika Kampuni ya FastJet PLC, 
Afisa Mwendeshaji Mkuu, Upande wa Airport, Alex Mjoge akizungumzia suala hilo la madai yao kama Wafanyakazi wa FastJet PLC. Kulia ni Mfanyakazi Mwandamizi ndani ya Ndege (Senior Cabin Crew) Mohamed Ngananya.
 Sehemu ya Wafabyakazi wa Kampuni ya Fastjet (Fastjet Plc)


*Waiomba Serikali chini ya Rais Dk. Magufuli kuingilia kati kuhakikisha haki inatendeka, 

* Wamshauri Masha akae kimya kwani naye ni mfanyakazi kama wao na anadai mshahara


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Fastjet(Fastjet Plc) nchini Tanzania wameiomba Serikali kuzishikilia ndege mbili za kampuni hiyo ili walipwe madeni yao ambayo wanadai kwa sasa yanayofikia Sh.Bilioni 2.75.

Wamesema kuna madai mengi ya fedha ambayo wafanyakazi wa Fastjet Plc walioko nchini Tanzania wanadai huku wakitoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Tano kuwasaidia ili wapate haki zao ikiwemo malimbikizo ya mshahara wanayodai.

Pamoja na kutoa kilio chao ,wafanyakazi hao wamesikitishwa na madai ambayo yametolewa na mfanyakazi mwenzao Laurance Masha ya kudai wafanyakazi wamelipwa mshahara wakati sio kweli kwani hata yeye naye anadai mshahara.

Wakizungumza leo Machi 6,2019 katika ofisi za Fastjet zilizopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ,wamesema katika kuhakikisha wanapata haki zinazostahili wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo ya kwenda kwenye mamlaka husika ambazo wanaamini zitawasaidia kupata haki zao.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wengine wa Fastjet zaidi ya 125, Mfanyakazi Mwandamizi ndani ya Ndege (Senior Cabin Crew) Mohamed Ngananya amesema kuwa kikubwa ambacho wanaiomba Serikali ni kuzishikilia Ndege mbili za Fastjet ambayo moja ipo nchini Tanzania na nyingine ipo Nairobi nchini Tanzania.

 "Tunapenda kutoa dukuduku letu kwa Serikali yetu ya Tanzania kuingilia kati na kutusaidia kupata madai na maslahi yetu kama wafanyakazi wa Tanzania toka kampuni Mama(Fastjet Plc) ambayo ndio mmiliki wetu mpaka leo hii tunazungumza na vyombo vya habari," amesema.

Ametaja baadhi ya madai yao ni malipo ya kisheria ya kuvunjwa kwa mkataba wa mfanyakazi ,malipo ya kisheria ya kiinua mgongo ya iliyokuwa Fly540 Tanzania Ltd, michango yao ya mifuko ya hifadhi (NSSF na PSSSF ya tangu Agosti 2018.Pia madai ya mshahara ya January 2019 ambayo baadhi yao wamelipwa nusu mshahara na kuahidiwa kulipwa kiasi kilichobakia baada ya wiki mbili lakini hawajalipwa mpaka leo.

Madai mengine ya wafanyakazi hao ni mshahara yao ya Februari 2019 ambayo haijalipwa kabisa."Tunaomba Serikali yetu kuzuia ndege mbili aina ya Embrear 190 zenye usajili wa Tanzania 5H- FJH na 5H-FJI na zisifutiwe huo usajili au kuruhusiwa kuondoka nchini kabla ya kulipwa madai yetu haya,"amesema Ngananya.

Ameongeza kuwa.menejinenti ya Kampuni yao hapa nchini Tanzania ulishawishi kutoa muongozo kwa Fastjet Plc kuwa kampuni hiyo ifungwe kwa taratibu zilizo rasmi na kisheria ili kuwezesha kila mfanyakazi na watoa huduma wote walipwe stahiki zao lakini hilo halikuzingatiwa na matokeo yake kusikia ghafla kuwa kampuni ya Fastjet Tanzania imeuzwa,hivyo wamtoa mwito kwa taasisi za Serikali kufuatilia kwa makini ununuzi huo.

" Zaidi Menejimenti ilitoa ushauri kwa mamlaka husika  TCAA ambayo inaratibu safari za anga na mashirika ya ndege hapa Tanzania kuwa wasitambue au kukubali mbadilishano huo wa umiliki wa kampuni hii hapa nchini kwasababu menejimenti haikuwa na taarifa za kina na za kutosha kuhusu uwezo wa kifedha kuendesha shughuli za usafirishaji abiria na kwa muda gani,"amesema.

Ngananya ameongeza kwanautaarifu umma wa Wa Tanzania kuwa kinachoendelea Fastjet Tanzania si kwasababu za kisasi kama wengi wanavyosema au kufikiria bali ni matatizo ya kiutendaji ya mwajiri wao mkuu ambaye ni Fastjet Plc kwa kutaka kukimbia madeni ambayo wanakataa kuyalipa madai yetu

"Tunaomba ujumbe kwa wafanyakazi wenzetu waliopo Zimbabwe na Msumbiji ,wachukue tahadhari ili mambo kama haya yasiwakute," amesema.

Alipoulizwa kuhusu Laurance Masha ambaye amekaririwa na baadhi ya vyombo kuwa wafanyakazi wa Fastjet wamelipwa mshahara,amejibu madai hayo hayana ukweli na kwamba hata yeye Masha naye mshahara wa Januari mwaka huu na mshahara wa February bado hajalipwa.

Alipoulizwa Masha ndio mmoja wa wanahisa,Ngananya amejibu kuwa wanachojua wao Masha ni mfanyakazi mwenzao kama walivyo wengine na wala hausiki na chochote ikiwemo ya kulipwa mishahara.

"Ni mfanyakazi kama tulivyo wengine tu,naye anadai kama sisi na hapa kwetu tunaye kiongozi wetu ambaye tunashirikiana kwa kila hatua ambayo tunaifanya ili kupata haki zetu,"amesema.

Kwa upande wake mfanyakazi mwingine ambaye ni Mkufunzi Ignace Tarimo amesema chini ya utawala wa Rais Dk.John Magufuli wanaamini haki yao itapatikana ingawa amesisitiza umuhimu wa Serikali kuzuia ndege hizo kwani ndizo zitawafanya wao wapate haki yao.

Wakati huo huo wafanyakazi wa Fastjet wamemshauri Masha ni bora akawa kimya badala ya kutoa kauli ambazo hazina ukweli na matokeo yake umma unapotoshwa kwa kupewa taarifa ambazo hazina ukweli.

Hats hivyo Masha mwishoni kwa wiki akizungunza na kituo cha Azam TV ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mambo ya kampuni hiyo ambapo aligusia suala la mishahara kuwa mishahara wa January umelipwa na mkakati wa kampuni hiyo ni kuingiza ndege sita.


Hivyo makala WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO

yaani makala yote WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wafanyakazi-fastjet-plc-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAFANYAKAZI FASTJET Plc NCHINI WACHARUKA,WAIOMBA SERIKALI KUZUIA NDEGE MBILI ILI WALIPWE FEDHA ZAO"

Post a Comment

Loading...