Loading...

UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?

Loading...
UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI? - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?
link : UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?

soma pia


UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?

Na  Moshy Kiyungi Dar es Salaam
 Kwa kawaida watu wamezoea kuona muziki wa dansi ukipigwa na wanaume na kuchezwa na watu wa jinsia zote. Kama ilivyo historia kwamba huwa haifutiki, inaeleza kuwa mwaka 1965, kundi jipya la aina yake lilianzishwa la ni bendi ya akina mama watupu, likapewa majina ya Women Jazz.

Akina mama hao wengine walikuwa ni wafanyakazi wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali (Government Press), walichaguana wenyewe kuunda bendi hiyo. Kina mama hao walipokuwa wakianza shughuli hiyo walikuwa hawana ujuzi wowote wa katika muziki, wakaanza kuhudhuria mafunzo ya muziki chini ya yule mwanamuziki mahiri Mzee Mayagilo.

Mayagilo kipindi hicho alikuwa kiongozi wa kitengo cha muziki Brass band katika Jeshi la Polisi, waanza mazoezi kwa nguvu. Bendi hiyo ilikuwa chini ya Umoja wa Vijana wa TANU (TANU Youth League) wakati ule. Sasa ni UVCCM.

Kutokana na jitihada zao wakajitengenezea utaratibu wa kuanza kufanya maonyesho yao hasa kwenye hafla za serikali na Chama tawala cha TANU wakati huo. Dhamira yao ilitimia Mei 31, 1966 ambapo bendi yao iliingia katika studio za RTD zilizopo jijini Dar es Salaam na kurekodi nyimbo zao sita.

Nyimbo hizo zilikuwa za Tumsifu mheshimiwa, Leo tunafuraha, Mwalimu kasema, Women Jazz, Sifa nyingi tuwasifu viongozi na TANU yajenge nchi. Women Jazz alikuwa ikiundwa na akina Mary Kilima, Juanita Mwegoha, Rukia Hassan na Siwema Salum ambao walikuwa waimbaji katika bendi hiyo.

Wengine ni Kijakazi Mbegu aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, Mwanjaa Ramadhani alikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na Chano Mohammed, aliyekuwa akipiga gitaa la kati la rhythm. Kwa upande wa ‘mdomo wa bata’ walikuwepo Tatu Ally na Anna Stewart waliokuwa wakipuliza Alto Saxophone, wakati Mina Tumaini na Rukia Mbaraka wakipuliza Tenor Saxophone.

Mama aliyejulikana kwa jina la Lea Samuel alikuwa akichangaya Bongos, wakati huohuo Josephine James alikuwa akidunda drums. Miaka hiyo kulikuwa na zana nyingi za muziki tofauti na miaka hii. Kulikuwepo na chombo kikiitwa Maracass kilichokuwa kilichezwa na Zainabu Mbwana wakati kile cha Timing alikuwepo Tale Mgongo.

Kwa wale wasioijuwa ama kukumbuka historia ya chama cha TANU, kirefu chake ni Tanganyika African National Union. Hicho ndicho kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hicho na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar, vilipounda Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.

Chama cha TANU kilianzishwa 7 Julai, 1954, kabla yake kulikuwepo na chama cha Tanganyika African Association (TAA). TAA ilikuwa na mwelekeo wa kitamaduni zaidi ya siasa. Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere. TANU ilikuwa ikishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961.

Katiba ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini, ikifuata mfano wa nchi za kijamaa zenye muundo wa siasa ya chama kimoja. Bendi ya Women Jazz ilipata umaarufu kiasi cha kuanza kufanya safari nje ya Tanzania, na kuweza kufanya maonesho katika miji ya Nairobi na Mombasa, baada ya kutembelea miji kadhaa hapa nchini.

Baada ya waaamuziki wa bendi hiyo kujiona hawapati faida yeyote kutokana na mapato ya bendi yao, wakiwa katika maandalizi ya kufanya ziara ya kwenda nchini China, bendi hiyo ilisambaratika. Nathubutu kutamka kwamba nyimbo za akina mama hao hazifahamiki kwa kizazi hiki kwa kuwa hakuna anaye jail kazi ya akina mama hawa. Hazichezwi katika kituo cha redio chochote hata TBC taifa iliyo na Maktaba kubwa ya muziki! 


Hivyo makala UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?

yaani makala yote UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI? mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/unafahmu-kuwa-wanawake-walikuwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?"

Post a Comment

Loading...