Loading...
title : UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA
link : UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA
UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema), akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kutokana na kutokuwepo kwa mbunge Aster Bulaya kwani amefanyiwa upasuaji.
Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza hayo leo Machi 28,2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo kesi hiyo ilikuwa inatakiwa kuanza kusikilizwa na kwamba wana mashahidi wawili na wako tayar lakini mshitakiwa Bulaya hayupo mahakamani.
Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala amedai mahakamani hapo kuwa Bulaya ana matatizo ya kiafya lakini ameridhia kesi hiyo kuendelea kusikilizwa bila ya yeye kuwepo.
Kutokana na hayo, mdhamini wa Bulaya, Ndeshukurwa Tungaraze amedai mshitakiwa huyo amefanyiwa upasuaji Machi 26, mwaka huu hivyo kutokana na hali yake ameshindwa kufika mahakamani.
Wakili Nchimbi amedai kama mshitakiwa ameridhia kesi hiyo iendelee kusikilizwa anatakiwa awasilishe taarifa kwa maandishi kuonesha kuridhia kwake.
Hakimu Simba amekubaliana na hoja za upande wa mashtaka, hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 17, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.
Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa Dk.Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa Zanzibar Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa Vicent Mashinji, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, John Heche na Mbunge wa Bunda Ester Bulaya.
Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama ambapo wote wanadaiwa kuwa February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.
Hivyo makala UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA
yaani makala yote UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/upasuaji-wa-ester-bulaya-wakwamisha.html
0 Response to "UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA"
Post a Comment