Loading...

UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI.

Loading...
UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI.
link : UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI.

soma pia


UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi akiwa amempakata mtoto Juma Abdul wakati jumuiya hiyo ilipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri jana katika maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani. Aliyesimama Katikati ni Mbunge wa Viti Maaalumu wa CCM Mkoa wa Pwani na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu. Msaada huo una thamani ya Sh.500,000.Picha Zote na Elisa Shunda
Picha ya Pamoja baada ya makabidhiano
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi (katikati) akizungumza na watoto wanaoishi maisha magumu na yatima wa kituo cha kulelea watoto cha Home Childrens jana,baada ya kuwakabidhi vitu mbalimbali katika maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani. Msaada huo una thamani ya Sh.500,000.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi (Kulia) akikabidhi msaada wa unga,sabuni na mafuta kwa uongozi wa shule ya sekondari ya Ikwiriri baada ya kuzungumza na wasichana wa shule hiyo iliyopo wilayani Rufiji jana. Msaada huo una thamani ya Sh.500,000.
Mwenyekiti wa UWT CCM Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi akizungumza na wasichana wa sekondari ya Ikwiriri juu ya kutambua thamani yao kusimamia malengo waliyojiwekea katika maisha yao.
Wakitembela Wodi ya Wazazi na Kujionea Changamoto Mbalimbali Zinazoikabili Kituo Hicho.

Viongozi wa UWT wakiwa pamoja na watoto wa Kituo cha Home Childrens kinacholea Watoto Wanaoishi katika Maisha Magumu na Watoto Wasio na Wazazi Yatima.




Kaimu Katibu wa Uwt Mkoa wa Pwani,Mwajuma Nyamka (katikati) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu wakati walipotembelea Kituo cha afya cha Ikwiriri jana.


NA:ELISA SHUNDA,RUFIJI


UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Pwani Wamewatembelea na Kutoa Msaada wa Sabuni ya Miche na Unga,Vyakula na Mafuta ya Kula Zenye Thamani ya Shilingi Laki Tano kwa Wanawake Waliolazwa katika Wodi ya Wazazi ya Kituo cha Afya cha Ikwiriri,Wanafunzi Wasichana wa Sekondari ya Ikwiriri na Kituo cha Watoto Yatima cha Childrens Home.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Pwani, Farida Mgomi alisema kuwa wapo katika wiki ya maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani ambacho kilele chake ni Machi 3 mwaka huu wao kama wakinamama wa mkoa wa pwani wameamua kuitumia wiki hiyo katika kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu na kutoa nasaha pamoja na kusikiliza changamoto zao ili kuwasaidia katika kuwakomboa wanawake na jamii kiuchumi,kisiasa na kifikra.

“Tumeamua kutumia wiki hii ya maadhimisho ya wanawake duniani kutoa misaada mbalimbali kwa watu maalumu wenye mahitaji ambapo katika maadhimisho haya sie uwt pwani tumewatembelea wodi ya wazazi na kuzungumza na wanawake kujua changamoto zao katika kituo cha afya cha ikwiriri,tumezungumza na wasichana wa sekondari ya ikwiriri juu ya kutambua thamani yao na kujitunza lakini pia tumetembelea kituo cha watoto waishio maisha magumu na yatima cha Ikwiriri tumekaa nao tumewasikiliza shida zao lakini pia kile tulichojaliwa kubeba tuliwapatia wenzetu kama njia ya kuwafariji na kuwaonyesha tupo pamoja nao;

“tumebahantika kuzungumza na wasichana wa sekondari ya Ikwiriri ambapo tumewaasa kuachana na masuala yote ya mtaani ikiwemo kurubuniwa na wanaume waishio karibu na shule hiyo,madereva bodaboda hata na walimu wao ili wapewe maksi nzuri lakini pia tumewaonya kutojipitisha pitisha na kuwatengenezea mazingira ya ushawishi walimu wao na mtaani kwa ujumla kwa kuvaa nguo zenye heshima na kuwa na staha katika shughuli zao ili waje kutimiza malengo yao tunatarajia kupitia wao tuje kupata viongozi wa ngazi za juu kama makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na wengineo” Alisema Mwenyekiti Mgomi.

Aidha Mwenyekiti Mgomi ameipongeza Serikali ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa,Dk.John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuipatia uongozi wa kituo cha afya cha Ikwiriri Shilingi Milioni 4 iliyowezesha uboreshaji na ukarabati wa majengo ya kituo hicho.

Aidha katika msafara huo wa uwt pwani waliongozana na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu Mbunge wa Viti Maalumu Anayetokea Mkoa wa Pwani alisema akiwa kama mbunge amepokea changamoto iliyosemwa na mganga mkuu wa kituo hicho na kusema bunge lijalo serikali itapeleka bungeni muswada wa kufanya bima ya matibabu badala kutibiwa sehemu uliyokatia utakuwa unahudumiwa mahali popote nchini.

“faida ya mabadiliko hayo hata upatikanaji wa dawa utaongezeka,na kwa mujibu wa takwimu walau kwa sasa dawa zinapatikana tofauti na awali hasa kwa zahanati na vituo vya afya ambavyo havidaiwi,ila nitalifikisha kwa mkurugenzi wa msd kuhusu watumishi pia naishukuru serikali yangu kwa mkoa wetu mwaka wa jana tumepata watumishi 248 kati ya walioajiliwa mi hatua nzuri” Alisema Mgalu

Akizungumza baada ya kuwapokea uongozi wa uwt,Mganga Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ikwiriri,Dk.Iddy Malinda aliishukuru serikali kwa kuwapatia fedha Shilingi Milioni 4 ambazo walizitumia katika uboreshaji wa majengo ya kituo hicho lakini pia kuna changamoto ya uhaba wa watumishi na vifaa tiba pamoja na madawa na kuiomba serikali ishughulikie suala hilo kwa kuwa kituo hicho kinahudumia wagonjwa wa aina mbalimbali kulingana na sehemu ilipo. 

Lengo la Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani ilitokea katika nchi za ulaya zilizoendela ambako wanawake waliamua kwa makusudi kupambana kutokana na uonevu waliokuwa wakiupata kwenye viwanda wengi wao waliuawa ndio maana siku hii ikawekwa kama kumbukumbu ya wapigania haki hao.


Hivyo makala UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI.

yaani makala yote UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/uwt-pwani-watoa-msaada-wa-shlaki-tano.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UWT PWANI WATOA MSAADA WA SH.LAKI TANO KWA WAZAZI,YATIMA NA WASICHANA WA SEKONDARI YA IKWIRIRI."

Post a Comment

Loading...