Loading...
title : UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA
link : UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA
UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA
Ubalozi wa Japan umeahidi kujenga Shule ya Sekondari ya kata ya Keikei ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya kata ya Busi inayohudumia wanafunzi wa kata mbili.
Ahadi hiyo ilitolewa na mwakilishi wa ubalozi wa Japan Bwana Takao Kurukawa katika kata ya Keikei alipofika katika eneo lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa sekondari hiyo hivi karibuni.
“Nimekuja kuangalia eneo ambalo litajengwa Shule ya Sekondari na ubalozi wa Japan baada ya kupokea maombi ya kuomba kujengewa shule kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa “Alisema Bwana Takao
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezeria Makota aliwashukuru ubalozi wa Japan kwa msaada wao na kuwataka wananchi wa Keikei kujitoa kwa hali na mali ila kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuwahudumia wananchi.
“Shukrani za dhati ziende kwa Mbunge Mhe.Ashatu Kijaji kutokana na agenda yake ya kuhamasisha elimu na sasa anatekeleza kwa vitendo baada ya kuona watoto wengi wanafaulu na kwenda shule ya Sekondari Busi hali iliyopelekea kuwa na upungufu wa madarasa hivyo mheshimiwa mbunge akaamua kwenda kuomba msaada ubalozi wa Japan na leo wamekuja.” Alisema Mhe.Makota
Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mustapha Semwaiko alisema kuwa katika Kata 21 za Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ni Kata ya Keikei pekee ambayo haikuwa na Sekondari ya Kata na kulikuwa na ufaulu mkubwa wa wanafunzi ambao ulisababisha msongamano katika Sekondari ya Busi na kupelekea kuwe na upungufu wa madarasa.
“Kutokana na kuwa na tatizo la madarasa Shule ya Sekondari ya Busi tulishirikiana na Mheshimiwa Mbunge tukapiga hodi katika ubalozi wa Japan ambao walikubali na watatujengea madarasa 8, matundu ya vyoo 10 na ofisi 2 za walimu na sisi tumetenga eneo la ekeri18 kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.”Alisisitiza Mustapha
Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Bwana Juma Ramadhani aliwashukuru viongozi wote walioshiriki katika kufanikisha jambo hilo kwa kuwa watoto wao walikua wakitembea umbali mrefu kufuata Sekondari katika kata jirani.
Hivyo makala UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA
yaani makala yote UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/ubalozi-wa-japan-kujenga-sekondari.html
0 Response to "UBALOZI WA JAPAN KUJENGA SEKONDARI KEIKEI KONDOA"
Post a Comment