Loading...

Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo

Loading...
Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo
link : Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo

soma pia


Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na wataalam wa Fiziotherapia wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu yalioandaliwa na Chama cha kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA). Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Scomt nchini Uholanzi, Prof. Willy Smeets na Rais wa APTA, Remla Mramba Shirima.
Baadhi ya wataalam wa Fiziotherapia wakimsikiliza Prof. Museru.
Mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Ellie Sawayael kutoka Hospitali ya DC Oltrumet mkoani Arusha, akimkabidhi zawadi mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi Liesbeth Westerih baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo leo.
Hivi ndivyo mmoja wa wataalam wa Fiziotherapia akifuatilia matukio mbalimbali leo.
Mtaalam wa Fiziotherapia wa Muhimbili, Bi. Eliela Kaaya amkimpatia keki Prof. Museru ikiwa ni siku ya kuzaliwa kwa Prof. Willy Smeets (kulia).
Rais wa APTA, Remla Mramba Shirima akimlisha keki, Prof. Willy Smeets kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Neema Tuwa kutoka Hospitali ya WAJA mkoni Geita akipokea cheti kutoka Prof. Museru baada ya kumaliza mafunzo hayo leo.
Mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Zamia Ladha wa Hospitali ya Gemsa Polyclinic jijini Arusha akipokea cheti kutoka Prof. Museru.
Prof. Museru akimkabidhi cheti mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Christabella Mugeu kutoka Hospitali ya Aga khan jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mafunzo hayo leo.
Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na wataalam hao leo.




Mafunzo ya siku tatu kwa wataalam wa Fiziotherapia nchini yamemalizika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku wataalam wakitakiwa kutumia elimu walioipata kuwasaidia wanaume na wanawake wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi, nyonga na mfumo wa mkojo

Pia, wanachama wa Chama cha kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) wametakiwa kutoa mchango wao katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na chama hicho kama vile kushiriki mara kwa mara katika shughuli za chama hicho.

Mkuu wa Chuo Kiku Cha Scomt nchini Uholanzi, Prof. Willy Smeets amemshukuru Mkuregenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru kwa kushiriki kikamilifu katika uandaji wa mafunzo hayo na kwamba ushiriki wake umeonyesha nia ya thati ya kuwajengea uwezo wataalam hao kutoka hospitali mbalimbali nchini.

“Mafunzo haya yamekuwa ya manufaa makubwa kwa wataalam hawa, ni imani yangu kuna mambo wamejifunza. Pamoja na kwamba tumetoa mafunzo kwenu, Prof. Museru napenda kukujulisha kwamba vifaatiba tulivyokuja navyo tunawapatia, tuwanawaachia ili mvitumie kutoa matibabu,” amesema Prof. Smeets.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru amewataka wataalam kuvitunza vifaa hivyo kwa kuwa vitakuwa msaada mkubwa kwa hospitali hiyo pamoja na wagonjwa.

Pia, Prof. Museru ametaka kuendelezwa kwa mazungumzo ya kuanzishwa kwa kozi ya shahada ya Fiziotherapia katika Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) ili kuandaa watalaam wengi zaidi na mkurugenzi huyo ameahidi kuunga mkono juhudi za kuanzishwa kwa shahada hiyo.

Washiriki wanatoka hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), CCBRT, Physiocare Arusha, London Health Centre, Police Barracks, Dar group Hospital, The Aga Khan Hospital -Dar es Salaam, GEMSA Polyclinic, Waja Hospital Geita na International Rescue Committee CBR ya mkoani Kigoma.



Hivyo makala Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo

yaani makala yote Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wafiziotherapia-wajengewa-uwezo-huduma.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo"

Post a Comment

Loading...