Loading...
title : WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
link : WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
Umoja wa wanawake wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wamedhamiria kuwakomboa wanafunzi wa kike wanao soma shule za sekondari zinazozunguka chuo hicho kwa kuwajengea mabweni ili kukuza kiwango cha elimu.
Wanawake hao wametoa ahadi hiyo wakati wakisherehekea siku ya wanawake duniani ambapo wameeleza kuwa sababu ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na changamoto nyingi zinazo wakabili wasichana na ikiwemo vishawishi vinavyosababisha mimba za utotoni jambo linalipelekea wanafunzi wengi kukatisha masomo yao.
Miongozni mwa shule ambazo zinazunguka chuo hicho cha Mzumbe ambacho ndio kinaongoza kwa ubora nchini ni pamoja na shule ya sekondari mongola, Adrian Mkoba, na kipela pamoja na shule ya msingi Mzumbe.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila terehe nane ya mwezi wa tatu kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Fikiri sawa, jenga uwezo na kuleta maendeleo endelevu.
Mgeni resmi katika mahadhimisho hayo, Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe.
Mgeni resmi katika mahadhimisho hayo Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa ya vitenge vya batiki vinazozalishwa na wajasiliamali wanawake wa kata ya bibwa manispaa ya morogoro.
Prof Aurelia kamuzola akitoa mada ya kuwahamasisha wanawake kujitambua na kuwa na hamasa ya kufikia malengo katika hafla ya kushrehekea maadhimisho ya siki ya wanawake duniani yaliyofanyika katika chuo kikuu cha mzombe mkoani morogoro.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe za siku wa wanawake duniani ambaye pia ni kuu wa kitengo cha maendeleo ya jinsia chuo kikuu cha mzumbe Dr Elizabeth Genda akitoa ahadi ya kujenga mabweni ya wasichana wa shule za sekondari zinazo zunguka chuo hicho.
Mwakilishi wa mgeni rasmi Bi Enedy Mwanokwate akipokea picha cha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina chonjo iliyochorwa na mmoja ya wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe katika hafla ya kusherehekea siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika chuo hicho.
Hivyo makala WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
yaani makala yote WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wanafunzi-chuo-kikuu-cha-mzumbe-mkoani.html
0 Response to "WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI"
Post a Comment