Loading...
title : Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa
link : Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa
Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa
Mtaalam wa Fiziotherapia, Beppie Hylkema kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi akitoa mafunzo kwa wataalam mbalimbali ambao wametoka hospitali mbalimbali nchini kuhusu tiba kwa kina mama na wanaume wenye matatizo kwenye mfumo wa mkojo, mfumo wa uzazi na maumivu katika nyonga. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Wataalam kutoka hospitali mbalimbali nchini nchini wakiwa kwenye mafunzo hay leo.
Mtaalam wa Fiziotherapia, Liesbeth Westerih kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi akijibu moja maswali kutoka kwa washiriki kuhusu matatizo yanayowapata kinamama katika mfumo wa uzazi wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo.Mmoja wa washiriki akiuliza swali kuhusu matatizo yanayowapata kinamama kwenye mfumo wa uzazi.
Baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika kutoa tiba kwa kinamama wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi.
……………………………………………………………………………………
Wataalam wa Fiziotherapia kutoka hospitali mbalimbali nchini leo wameanza mafunzo kuhusu tiba afya eneo la nyonga, mfumo wa mkojo na mfumo mzima wa uzazi kwa kina mama.
Mafunzo hayo ambayo ni ya siku tatu yanaendeshwa na Chama cha kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) kwa kushirikiana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini uholanzi.
Katibu wa chama hicho, Bw. Abdallah Makalla amesema mafunzo hayo yamelenga kuinua kiwango cha utoaji huduma kwa wataalam wa fiziotherapia katika eneo hilo ili waweze kutoa huduma ya ubobezi wa juu kwa kinamama na wanaume wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo na eneo la nyonga.
Mtaalam wa Fiziotherapia, Liesbeth Westerih amesema wataalam hao wanapaswa kutumia vifaa maalum kwa ajili kutibu kina mama na wanaume wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo, mfumo wa haja kubwa, viungo vinavyozungukwa na nyonga na wenye maumivu ya nyonga.
Pia, wataalam hao wamepatiwa mafunzo ya kutumia vifaa maalum kwa kinamama wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi na wale wanaopata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Washiriki katika semina hiyo wamefundishwa jinsi ya kutibu kina mama wenye matatizo kwenye eneo la nyonga na mfumo wa uzazi kwa kutumia njia mbalimbali kitaalamu kama vile kufanya uchunguzi na kutoa ushauri kwa wagonjwa kabla ya kupatiwa tiba.
“Wewe ni mtaalam, hakikisha unaelwa historia ya mgonjwa, fanya uchunguzi ili kujua unamtibu mgonjwa wa aina gani, jua sababu za ugonjwa wake na pia hakikisha unamshauri kiasi kwamba mgonjwa anakuelewa vizuri,” amesema Mtaalam wa Fiziotherapia, Beppie Hylkema kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwajengea uwezo wataalam hao ambao watatoa tiba kwa kinamama nchini ili kukabiliana na ongezeko la matatizo kwa kinamama wajawazito na wale waliojifungua.
Washiriki wanatoka katika hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), CCBRT, Physiocare Arusha, London Health Centre, Police Barracks, Dar group Hospital, The Aga Khan Hospital -Dar es Salaam, GEMSA Polyclinic, Waja Hospital Geita na International Rescue Committee CBR ya mkoani Kigoma.

Hivyo makala Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa
yaani makala yote Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wataalam-wa-fiziotherapia-nchini.html
0 Response to "Wataalam wa Fiziotherapia nchini wapigwa msasa"
Post a Comment