Loading...
title : Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi
link : Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi
Na Issa Mtuwa – Wizara ya Madini Tarime
Waziri wa madini Mhe. Doto Biteko ameonyesha kukerwa na tabia zinazofanywa na uongozi wa juu wa mgodi wa Acacia North Mara kwa serikali kwa kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vinavyo andaliwa baina ya pande hizo mbili, licha ya baadhi ya vikao kuongozwa na Waziri wa Madini lakini viongozi wa juu wa mgodi ambao ndio wafanya maamuzi na watekelezaji wa maagizo ya serikali wamekuwa wakishindwa kuhudhuria .
Biteko amesema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara jana Machi 5, 2019 katika kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi kwenye migodi ya North Mara na Buhemba. Biteko amesema anakerwa na tabia za uongozi wa mgodi huo kwa kushindwa kuhudhuria mara kwa mara mikutano mbalimbali ya ndani na ile ya hadhara badala yake wamekuwa wakituma wawakilishi.
“ Kuanzia leo, haki ya mungu, haki ya mungu, haki ya mungu, mimi Waziri wa Madini leo ni siku ya mwisho kukaa na hawa wawakilishi kwenye vikao, hasa kama hivi vinavyo husu hatima ya maisha ya watu alafu wafanya maamuzi hawahudhurii. Niwambie ukweli nasikitishwa sana na tabia hii. Hawa walipo sio saizi yangu, kama ni hawa hata mimi ningewaleta maafisa wa wizara tena wale wanaolingana na hawa.
Wanataka wawepo hadi afike Rais…!? nendeni mkawambie kwenye ngazi ya Wizara mimi ndio wamwisho katika kufanya maamuzi, kama mimi nipo kwa nini wao wasiwepoo…!? nyinyi mliokuja hapa nendeni mkawaambie hii ni mara ya mwisho wasifikiri serikali hii wanaweza kuiweka mfukoni, haikubaliki, hii tabia lazima ifike mwisho” alisema Biteko huku akisikitika sana.
Amesema kwa ujumla hafurahishwi na namna mambo yanavyokwenda mgodini hapo ukilinganisha na migodi mingine. Mgodi wa North Mara umezungukwa na matatizo mengi sana yakiwemo ya malipo yafidiaza wananchi, utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekiiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wa kwanza kushoto akitoa taarifa fupi ya hali ya mkoa wake wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tarime.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akionyesha kwa kuuliza mwisho wa mpaka wa eneo la ujenzi wa TSF mpya, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya Tarime.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa tatu kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara wakielekea kwenye eneo la uchimbaji wa TSF kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Kighoma Malima
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa tatu kulia akiteta jambo na Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe. John Heche wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nyamong wilayani Tarime katikati yao ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime.
Hivyo makala Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi
yaani makala yote Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-wa-madini-mhe-doto-biteko.html
0 Response to "Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko atembelea Tarime, asirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi"
Post a Comment