Loading...

WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

Loading...
WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI
link : WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

soma pia


WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.

Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
Kamishna wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.


Hivyo makala WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

yaani makala yote WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-biteko-ateta-na-wenye-nia-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI"

Post a Comment

Loading...