Loading...

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

Loading...
WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III
link : WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

soma pia


WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka. Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika. Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.
Mhandisi huyo alisema tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali na kwamba mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo linauwezo kubeba abiria milioni sita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Terminal Three, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Hivyo makala WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

yaani makala yote WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-mkuu-aridhishwa-na-hatua-za.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III"

Post a Comment

Loading...