Loading...

WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Loading...
WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA
link : WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

soma pia


WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuna faida nyingi ambazo zinapatikana katika utoaji wa huduma za afya nchini kwa kutumia mifumo ya teknolojia iliyopo.

Ameyasema hayo leo Machi 27,2019 wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Afrika Mashariki ambao unazungumzia utoaji huduma za afya kidigitali ambapo kupitia mkutano huo watalaam wa kada mbalimbali wanatangalia jinsi gani teknolojia inaweza kutatua changamoto katika sekta hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kukua kwa teknolojia kumesaidia katika utoaji wa huduma za afya nchini ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea kupitia uwepo wa teknolojia madaktari bingwa katika masala ya uzazi wameanzisha kundi lao kwenye WhatsApp na wanalitumia kwa ajili ya kusaidiana katika mambo yanayohusu uzazi.

"Kundi hilo limewaunganisha madaktari wote waliobobea katika eneo la huduma zinazohusu  uzazi, kupitia kundi hilo madaktari wanapohitaji msaada wowote kwa mama anayejifungua inakuwa rahisi kuupata.

"Kupitia kundi hilo tunayo taarifa kuwa imesadia kuokoa maisha ya mama na mtoto.Hivyo kwetu sisi tunaiangalia teknolojia kama sehemu sahihi ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini,"amesema.

Pia amesema kupitia uwepo wa teknolojia hivi sasa katika maeneo mengi ya utoaji wa huduma za afya mifumo mingi inatumia teknolojia akitolea mfano kwa sasa taarifa za mgonjwa zinawekwa katika kompyuta badala ya kuweka kwenye mafaili kwa kuandikwa kwenye karatasi.

"Tunaendelea kuhamasisha watoa huduma za afya kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa teknolojia, wapo baadhi bado wanaweka taarifa za mgonjwa kwenye faili na matokeo yake baada ya kuandika anaanza tena kuhamisha kwenye kompyuta na hivyo kujipa kazi mara mbili,"amefafanua Waziri Ummy

Pia amesema  kwa Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha kunakuwa na mifumo imara ya kidigitali inayorahisha utoaji wa huduma za afya.

Kuhusu mkutano huo  ulioanza leo jijini Dar es Salaam na kuendelea kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Ummy amesema umezikutanisha nchi tano za Afrika Mashariki na kwa sehemu kubwa wanaangalia sekta ya afya na uwepo wa mfumo wa utoaji huduma za afya kidigitali.

"Katika mkutano huu kuna mambo mengi yatajadiliwa kuhusu kutumia mifumo ya digitali katika kutoa huduma za afya. Tutaangalia uwepo wa changamoto zinazopatikana wakati wa utoaji huduma za afya kwa kutumia mifumo ya kidigitali na kisha kutafua ufumbuzi wake,"amesema.

Kupitia mkutano huo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua mfumo wa kidigal katika utoaji wa huduma za afya ambapo amesema utasaidia kurahisisha utoaji huduma kwani madaktari watakuwa wakitoa huduma hata kama hawapo eneo husika ilimradi wapo kwenye mfumo huo.

"Mfumo huu wa kidigitali tuliouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi zetu za Afrika Mashariki kwani madaktari watakuwa na uwezo kuwa kumtibu mgonjwa kwa kutumia mfumo huu,"amesema Mama Samia na kuongeza Tanzania inapaswa kwenda kasi zaidi katika kuutambulisha mfumo huo na kuutumia.

Wakati huohuo Waziri wa Afya kutoka nchini Burundi Thadde'e Ndikumana amesema mfumo wa kidigitali umekuja wakati muafaka na kufafanua katika nchi yao wamekuwa wakitumia zaidi Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Nairobi nchini Kenya pindi raia wao wanapohitaji kutibiwa.

Hivyo baada ya kuzinduliwa mfumo wa kidigital katika kutoa huduma za afya watakuwa na nafasi ya kuwatibu wagonjwa walioko kwenye nchi yao bila kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili au Nairobi."Kwa kutumia mfumo huu sasa watu wetu watabiwa na madaktari wa Muhimbili au Nairobi bila ya kwenda huko."


Hivyo makala WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

yaani makala yote WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waziri-wa-afya-aelezea-umuhimu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA"

Post a Comment

Loading...