Loading...
title : Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni
link : Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni
Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni
Mkurugenzi Kitengo cha Mauzo ya Fedha za Kigeni wa Benki ya
Barclays Tanzania, Esther Maruma (katikati), akizungumza na waandishi
wa habari, Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa duka la
kubadilishia fedha za kigeni la benki hiyo. Wengine kushoto ni, Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano, Aron Luhanga na Mkuu wa Kitengo cha Wateja
Binafsi, Oscar Mwamfwagasi.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania,
Oscar Mwamfwagasi (mbele kulia), akizungumza na waandishi wa habari,
Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa duka la kubadilishia fedha za
kigeni la benki hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo
ya Fedha za Kigeni, Esther Maruma na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano,
Aron Luhanga.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo ya Fedha za Kigeni wa Benki ya
Barclays Tanzania, Esther Maruma (wa pili kulia), akishikana mikono na
Meneja Mauzo wa Hoteli ya Serena, Shaban Kaluse wakati wakizindua
rasmi duka la kubadilishia fedha za kigeni la benki hiyo jijini Dar
es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Oscar
Mwamfwagasi na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Barclays, Aron
Luhanga.
KATIKA kuunga mkono juhudi za Benki Kuu ya Tanzania ya kuhakikisha huduma ya kubadilishia fedha za kigeni inafanyika kwa kufuata sheria na vilevile hakuna uhaba kwa wataohitaji huduma hiyo, benki ya Barclays Tanzania imefungua kituo cha kubadilishia fedha katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Uhaba wa sasa unatokana na uamuzi wa Benki Kuu kufunga maduka ya fedha yanayokiuka sheria za endeshaji , na kuyataka mabenki - ambayo kimsingi yamekuwa yakibadilisha fedha za kigeni katika matawi yao - kujikita rasmi sasa kutoa huduma hiyo kwa kiwango kinachokidhi utashi wa soko.
Akiongea katika uzinduzi huo, Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo ya Fedha za Kigeni wa Barclays Esther Maruma alisema, “ Mkakati huu unalenga kukidhi haja za ubadilishaji wa pesa za kigeni taslimu, ili kuziba uhaba unaotokana na maduka ya fedha kufutiwa leseni zao za biashara. “
Alisema ufunguzi huo ni mwanzo wa mkakati wa benki hiyo kupanua wigo wa huduma hiyo, na kwamba vituo zaidi vitafunguliwa katika siku za usoni, ili kuwapa nafasi wateja wanaotaka kubadilisha fedha kwa njia ya halali kupata huduma hiyo kwa urahisi na kwa gharama nafuu zaidi.
Akitoa ushuhuda wa ukubwa wa uhaba wa huduma hiyo, Meneja wa Mauzo wa Serena, Shaban Kaluse alisema walilazimika kutenga fedha na kuziweka kibindoni float), ili kuwapa mkopo wateja wao ambao walikuwa wanajikuta wanahitaji fedha za kigeni nyakati ambazo mabenki nayo yamekwisha fungwa.
Kituo hicho cha Serena kwa kujibu wa Kaluse kipo katika eneo lenye uhitaji mkubwa sana wa huduma za kubadilisha fedha za kigeni jijini Dar es Salaam. Akiongelea huduma za kituo hicho, Mkuu Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Barclaya Aron Luhanga alisema kitafanya kazi siku saba kwa wiki.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Barclays, Oscar Mwamfwagasi alisisitiza kuwa huduma hiyo ya kubadilisha fedha itafanyika kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo, ikiwemo wateja kuonyesha vitambulisho na uthibitisho wa haja ya kupata fedha za kigeni kwa wanaotarajia kusafiri.
Uamuzi wa Benki Kuu kuhamisha imani ya kufanya biashara za ubadilishaji fedha za kigeni kwenda kwa mabenki ya biashara unafuatia operesheni ya ukaguzi wa maduka ya fedha za kigeni uliofanywa na hiyo, ambao uligundua kuwepo kwa ukiukaji mkubwa wa taratibu na kanuni za uendeshaji.
Katika kutilia mkazo uzito wa ukiukaji wa taratibu uliobainishwa kwenye operesheni hiyo, hivi karibuni Rais Dr. John Magufuli alisema moja ya sababu za kuyafunga maduka mengi ya kubadilishia fedha za kigeni ni baada ya kugundulika yalikuwa yamegeuka vichochoro vya kutoroshea fedha nje ya nchi.
Hivyo makala Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni
yaani makala yote Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/barclays-yaitikia-wito-wa-bot-yafungua.html
0 Response to "Barclays yaitikia wito wa BoT, yafungua duka la kubadilishia fedha za kigeni"
Post a Comment