Loading...

MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

Loading...
MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA
link : MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

soma pia


MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza ofisini kwake mjini Babati.
……………………….
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema sekta ya afya ni nyeti isiyopaswa kuingiliwa na wanasiasa ila madaktari na wauguzi wanapaswa kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwemo kuzuia vifo vya mama na mtoto.
Mnyeti aliyasema hayo mjini Babati, wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, madaktari na wauguzi kwenye uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama. 

Alisema kazi ya viongozi ni kusimamia utekelezaji na madaktari na wauguzi wafanye kazi zao kwa vitendo huku wakitumia lugha nzuri pindi wanapotoa huduma kwa wagonjwa. Alisema wataalamu wa afya wanapaswa kutimiza wajibu wao katika uwajibikaji na kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga waweze kuwa watu wazima. 

“Kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anatimiza jukumu lake ikiwemo kupatiwa huduma bora ili kudhibiti vifo vya kina mama na watoto pamoja na kutoa elimu kuanzia ngazi ya jamii,” alisema Mnyeti. Alisema kwa mujibu wa sera za afya nchini, huduma za uzazi hutolewa bure ila kuna baadhi ya maeneo malalamiko ya mama wajawazito kudaiwa fedha yamekuwa yakitolewa. 

“Halmashauri na wengineo kasimamieni hilo inawezekana suala la kuwatoza fedha wajawazito au wa mama waliojifungua halipo kwetu ila lichunguzwe na kufanyiwa kazi,” alisema Mnyeti. Mkazi wa mjini Babati, Aloyce Bura aliiomba serikali kuhakikisha wanaboresha huduma kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) ikiwemo upungufu wa watumishi na dawa. 

Bura alisema wakati huu ambapo serikali inaboresha huduma za afya ikiwemo kujenga vituo vya afya na hospitali za wilaya inapaswa kuongeza watumishi na dawa. Mkazi wa mtaa wa Miyomboni, Mariam Sulle aliwapongeza wauguzi wa hospitali ya Mrara kwa kuwa na lugha nzuri kwa wanawake wajawazito pindi wanapowahudumia tofauti na awali. 


“Mgonjwa anahitaji faraja na lugha nzuri, niwapongeze kwa kutoa huduma zao ipasavyo kwani ukitoa lugha mbaya mgonjwa anaona bora akafie nyumbani kwao kuliko kutukanwa hospitalini,” alisema Sulle.


Hivyo makala MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

yaani makala yote MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/mnyeti-azindua-kampeni-ya-jiongeze.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA"

Post a Comment

Loading...