Loading...
title : WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI
link : WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI
WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI
Na Ahmed Mahmoud,Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr.Anna Mghwira amewataka Wazalishaji wa mifuko mbadala ambayo ni rafiki wa mazingira kuchangamkia fursa ya kuzalisha kwa wingi mifuko na kukidhi mahitaji ya mifuko kwani tayari mkoa huo umepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mghira alisema hayo akitembelea maonyesho ya wiki ya elimu katika uwanja wa Mashujaa Wilayani Moshi ,amesema kuwa wajasiriamali wanaotumia vifungashio vya mifuko ya plastiki wanapaswa kujiianda mpaka muda uliopangwa na serikali Mwezi June mwaka huu waweze kuondokana na matumizi ya plastiki.
“Kwa sasa mkoa wa Kilimajaro ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki tumeanza mapema ili watu wajiandae ikifika mwezi wa sita mwaka huu watu wawe kwenye mstari na kuzoea kutumia mifuko mbadala tunashukuru wenzetu wa Harsho Group wameanza kuzalisha mifuko ya kutosha ” Alisema Dr.Anna
Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro wamejianda vyema kuzalisha mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira na kuisambaza kwa bei nafuu.
Caroline alisema kuwa wanazalisha mifuko laki 5 kwa siku ambayo inatosheleza mahitaji ya mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani pamoja na Tanzania nzima hivyo wamejiandaa kuzi ba pengo la mifuko ya plastiki.
Anaeleza kuwa mifuko hiyo inaweza kufuliwa zaidi ya mara tano na iwapo ikitupwa inaweza kuoza na kuwa mbolea katika ardhi.
Mkazi wa Manispaa ya Moshi Roman Mnzava alisema kuwa hatua ya Mkoa wa Killimanjaro kupiga marufuku matumizi ya plastiki utasaidia kuokoa mazingira na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni kitovu cha utalii mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr.Anna Mghwira
Hivyo makala WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI
yaani makala yote WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/wazalishaji-mifuko-mbadala-kuziba-pengo.html
0 Response to "WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI"
Post a Comment