Loading...
title : MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD
link : MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD
MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD
Na Humphrey Shao, Michuzi TV
Jopo la Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lililokuwa likimfanyia Uchunguzi Mwanadada Mariamu Rajabu kuhusu kidonda chake cha Mgongoni limekubalina kwa pamoja kumuamishia mgonjwa huyo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ibrahim Mkoma amesema kuwa mara baada ya jopo la madaktari wa Hospitali ya Tiafa Muhimbili kufanya uchunguzi kwa kina wameamua kumpa rufani mgonjwa huyo kwenda hospitali ya Ocean Road hili aweze kupata matibabu zaidi.
Hata hivyo waandishi wa habari walipohoji nini matokeo ya uchunguzi wa na kwanini wanamuamishia katika Hospitali ya Saratani Dk Mkoma alikataa kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi wake na kusema kuwa matokeo hayo ya ugonjwa huo ni siri ya Daktari na Mgonjwa kama kanuni za kitabibu zinavyohitaji.
Hata hivyo Globu ya Jamii ilipomuuliza Mariamu Rajabu juu ya ugonjwa wake alisema kuwa awezi kuzungumzia ugonjwa huo kwa sasa na hayupo tayari kuzungumzia ugonjwa wake.
Muhimbili (MNH) ilianza kumfanyia uchunguzi Mariam Rajab kubaini chanzo cha kidonda alichonacho mgongoni. Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kufuatia kidonda hicho kilichodumu kwa muda mrefu.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari amesema hospitali hiyo imechukua jukumu la kumtibia Mariam baada ya kupata maelekezo kutoka wizara ya afya na serikali itabeba gharama zote.
Alisema waliona ile video nakufanya juhudi za kumtafuta na hatimaye ametoka Singida na kukaa naye wodini, kwa matibabu yanaendelea na tayari madaktari wamechukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mariam alieleza kuwa kidonda hicho amekuwa nacho kwa muda mrefu na amekuwa akikitibia mara kwa mara ila Agosti 2018 kimefuka upya na kumsababishia maumivu makali. Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo Mariam anatakiwa kupatiw
Mwanadada Mariamu Rajabu akiwa amelala kwenye kitanda akisaidiwa na muhudumu wa afya katika hospitali ya Tiafa Muhimbili.
Jopo la Madaktari waliokuwa wakimuhudumia Mwanadada Mariamu Rajabu aliyelala kwenye kitanda katika hospitali ya Tiafa Muhimbili.
Hivyo makala MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD
yaani makala yote MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/muhimbili-kumuamishia-mariamu-rajabu.html
0 Response to "MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD"
Post a Comment