Loading...

WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja

Loading...
WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja
link : WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja

soma pia


WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Jamala Adam Taib (kushoto) akisaini Mkataba wa ununuzi wa Mashine ya City Scan mpya kwa ajili ya Hospitali ya Mnazimmoja, kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Pacific Diagnostic Ltd ya Dar es Salaam Brian Kamuzora. Hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Zanzibar Amina Muhammed Jabir akikagua Mkataba wa ununuzi wa City Scan mpya uliosainiwa leo April 4, Mashine hiyo itagharimu Dola Laki nane. Picha na Makame Mshenga.
Na Fatma Kassim, Afya.
WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini Mkataba wa manunuzi wa mashine mpya ya CTscan na kampuni ya Pacific Diagnostic Ltd ya Dar es Salaam yenye thamani ya dola laki nane.
Mkataba huo umehusisha ununuzi, uletaji, ufungaji pamoja na utoaji wa mafunzo ya CT scan kwa Watendaji wa Wizara ya Afya.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt Jamala Adam Taib amesema kuwa kupatika kwa mashine hiyo mpya ya CTscan ni hatua kubwa ya mafinikio kwa Zanzibar ambayo itwasaidia wananchi katika kuchunguza maradhi mbali mbali.
Amesema Serikali imeona ipo haja ya kununua mashine hiyo mpya kwa sasa kutokana na kuongezeka kwa huduma mbali mbali za afya zinazotolewa hapa nchini ambazo zinahitaji uchunguzi wa kina na waharaka katika mahospitali.
Amesema mashine hiyo itakuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia ambapo inatoa slide 128 kwa wakati mmoja ukilinganisha na iliyokuwepo hivi sasa katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo imefikia miaka 10 hivi sasa.
Alifahamisha Fedha zilizotumika kununulia mashine hiyo ni za Serikali kwa asilimia mia moja ambapo alisema ni juhudi kubwa zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein za kuhakikisha sekta ya Afya inakuwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wanapata huduma zenye ubora.
Dkt Jamala alisema tangu kuanza kwa hatua ya kuwepo kwa mashine ya CTscan kwa Hospitali ya Mnazimmoja kumesaidia kuwepo kwa huduma nyingi ikiwa na pamoja na kuja kwa Madaktari wa kichwa na Mgongo kutoka nje ya nchi ambapo wanasaidia na madaktari Wazalendo katika kuwapatia matibabu hapa nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Kampuni ya PACIFC DIAGNOSTIC LTD Brian Kamuzoka ameihakikishia Serikali kuwa mashine ambayo wataileta hapa nchini ya CTscan ni yenye ubora na aina ya mashine hiyo inatumika Hospitali kubwa duniani kote.
Amesema baada ya kuifunga mashinene hiyo watakuwa na mkataba maalumu wa kuifanyia mataengenezo pamoja na kuisimamaia ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.


Hivyo makala WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja

yaani makala yote WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/wiizara-ya-afya-zanzibar-kununua.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WIizara ya Afya Zanzibar Kununua Mashine ya CT Scan Mpya Hospitali ya Mnazi Mmoja"

Post a Comment

Loading...