Loading...
title : OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU
link : OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU
OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
IMEELEZWA kuwa binadamu kukang'atwa na mdudu nyuki kuna faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo ya kusaidia kuondoa sumu mwilini, hivyo kwa wale ambao watang'atwa hawana sababu ya kumuua nyuki.
Hayo yameelezwa na Ofisa Ugugaji Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Rueben Nyambita wakati anazungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe pamoja na Shule ya Sekondari Pugu ya jijini Dar es Salaam ambapo TFS imeamua kuzungumza na wanafunzi hao kwa lengo la kuwapa elimu inayohusu utunzaji wa misitu , faida za uwepo wa misitu na ufugaji nyuki katika misitu mbalimbali chini.
Hivyo TFS imeamua kuja na mkakati wa kuhakikisha inazungumza na wanafunzi mbalimbali kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo ambapo wanaamini wakiipata vema elimu kuhusu utunzaji misitu na rasilimali za misitu watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine.Hivyo maofisa wa kada mbalimbali wa TFS walienda katika shule hizo kuzungumzia misitu na faida zake pamoja na utalii unaopatikana ndani ya hifadhi za misitu ikiwemo ya asili na hasa ambayo iko chini ya TFS.
Wakati wanazungumza na wanafunzi hao kwa nyakati tofauti, Nyambita pamoja na kuzungumzia faida nyingi zinazopatikana kutoka kwa mdudu nyuki akatumia nafasi hiyo kueleza iwapo binadamu atang'atwa na nyuki, basi sumu iliyokuwa mwili itaondoka."Kukang'atwa na nyuki kuna faida, hivyo ukiona amekung'ata mahali ujue anakwenda kuondoa sumu na tunatarajia kuwa uvimbe wake hauwezi kuwa mkubwa."
Nyambita ameongeza hata kama binadamu ataumwa na nyuki watatu, wanne, watano au hata 10 bado watasaidia kundoa sumu na iwapo mhusika atavimba sana kuliko kawaida maana yake mwili wake utakuwa na sumu nyingi , hivyo inapokutana na sumu ya nyuki inasababisha aleji.
Hata hivyo amefafanua nyuki anayo sumu lakini haina madhara sana kwa binadamu zaidi ya tiba lakini iwapo binadamu ataumwa na nyuki wengi sana kwa wakati mmoja basi ni rahisi kupata madhara kwani sumu ya nyuki itakuwa nyingi mwilini."Wanafunzi na wananchi kwa ujumla msigope kuumwa na nyuki kwani ni sehemu ya tiba."
Kuhusu asali inavyotengenezwa, Nyambita amewaambia wanafunzi hao kuwa, asali ya nyuki inatengenezwa kutokana na mimea mbalimbali ambayo nyuki hupendelea kwenda kufyonza maji na hasa kwa maua ambayo yanatoa maji yenye ladha ya sukari.
"Asali ya nyuki inatengenezwa na sukari ambayo inaitwa glukosi inayopatikana kwenye mimea mbalimbali.Nyuki anapotua kwenye mmea anavyonza maji na kisha anachuja sukari inayopatikana kwenye ule mmea ambayo ni kati ya asilimia 25 hadi 40 maji ya mimea hiyo inakuwa na sukari.Pia nyuki mwenyewe anavyo vimeng'enya vya kutengeneza asali kwa asilimia 75 hadi asilimia 80,"amesema Nyambita.
Alipoulizwa na wanafunzi hao kwanini asali inaganda, amewajibu inatokana na glukosi ambayo ipo kwenye asali na ndio maana inasababisha kuganda na kuganda haina maana imeharibika.Kuhusu rangi tofauti ya asali , amesema hiyo inatokana na mimea ambayo nyuki ameifikia na kwa kuwa mimea ina rangi tofauti ni jambo la kawaida asali nayo kuwa na rangi tofauti tofauti.
Wanafunzi hao wameelezwa kuwa nyuki anapotengeneza asali, kwa kawaida anatengeneza kwa ajili ya chakula chake kwa kutambua kuna nyakati za ukame na njaa na hivyo anajiandaa kwa kuwa na chakula cha akiba lakini binadamu kwa uroho wao wameamua kula chakula cha nyuki ambayo ndio hiyo asali inayopendwa na watu wa rika mbalimbali.
Pia amesema kuna maziwa ya nyuki na hayo ni maalumu kwa ajili ya kulishwa malkia wa nyuki kutokana na jukumu ambalo analifanya kwa nyuki wengine, huku ikielezwa maziwa ya nyuki yana protini nyingi na kwa mwenye kuitumia anakuwa na akili nyingi sana na kama ni mwanafunzi atakuwa anafanya vizuri kwenye masomo kwa kushika nafasi za juu.
"Wanafunzi na Watanzania wenzangu kwa ujumla niwaambie tu kuna faida nyingi sana za uwepo wa nyuki , hivyo ni vema tukahakikisha tunazalisha kwa wingi mazo ya nyuki ambayo yanaweza kutuingizia kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.Kuna aina mbili za kufuga nyuki ikiwemo ile ya asili na ya kisasa lakini hii ya kisasa ambayo ni kutumia mzinga nyuki wanatoa asali nyingi zaidi,"amesema Nyambita.
Pamoja na hayo yote TFS kupitia maofisa wake ambao walikuwa sehemu ya kwenda kuzungumza na wanafunzi hao wametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina kuhusu umuhimu wa kufidhi misitu ya asili na kuhamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani wa kutembelea hifadhi hizo.
Hivyo makala OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU
yaani makala yote OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/ofisa-ufugaji-nyuki-wa-tfs-asema.html
0 Response to "OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU"
Post a Comment