Loading...
title : TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU
link : TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU
TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umeweka mkakati kuhakikisha inatoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani na Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam kwani wanaamini iwapo wanafunzi hao watakuwa na uelewa mzuri kuhusu misitu iliyopo watakuwa mabalozi wazuri na walinzi wa misitu nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hizo kwa nyakati tofauti, Meneja Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Mariam Kobero amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuhakikisha misitu yetu nchini inalindwa na kudhibiti uharibifu wa mazingira na katika jitihada hizo hizo TFS nayo imekuwa na mikakati ya kufanikisha misitu nchini inatunzwa na kulindwa wakati wote.
Kobero amesema kwa kutambua umuhimu na faida za misitu TFS imeona ni vema ikakutana na wanafunzi wa shule hizo kwa lengo la kutoa elimu ambayo itajikita zaidi kuelezea faida za misitu na umuhimu wa kuilinda kwani ili misitu iwe salama ni jukumu la kila Mtanzania kuwa mlinzi ikiwa pamoja na kutokuwa tayari kuona msitu unaharibiwa halafu anakaa kimya.
"Wakala wa Huduma za Misitu hatujalala, tunatambua pamoja na mambo mengine ni wajibu wetu kukutana na makundi ya watu mbalimbali ili kutoa elimu inayohusu umuhimu wa misitu kuilinda na kutokata miti hovyo.Hivyo leo hii tumeamua kuzungumza na wanafunzi wetu hao ambao tunaamini watakuwa mabalozi wetu waa wazuri kwa wananchi wengine.
"Pia wanafunzi hawa tunawaleza si tu kuhusu misitu tuliyonayo bali tunawaeleza na uwepo wa fursa ya kufanya utalii wa ndani kwa watanzania kwani katika misitu yetu kuna vivutio mbalimbali. Kwa hapa Pugu tu , katika kilele cha Mlima Pugu ukienda unauona mji wote wa Dar es Salaam.Watalii wengi kutoka nje wanakuja , hivyo tunawaambia wanafunzi wafahamu na wao watawafahamisha wengine," amesema Kobero.
Alipoulizwa iwapo ipo haja ya kuwa na mitaala inayozungumzia kwa kina kuhusu misitu na mazao yatokanayo na misitu pamoja na utalii, Kobero amesema anatambua uwepo wa masomo yanayozungumzia kuhusu faida za misitu na utalii lakini kwake anaona ni vema ukaweka msisitizo zaidi kwa kuweka masomo yaliyojikita katika maeneo hayo ili kuwajengea wanafunzi uelewa mpana zaidi.
Kuhusu iwapo elimu hiyo ambayo imetolewa kwa wanafunzi wa Sekondari ya Pugu na Minaki, Kobero amesema mkakati wa TFS ni kuhakikisha kanda zote kunakuwa na utaratibu huo na kwamba waaamini watawafikia wanafunzi wengi zaidi pamoja na makundi ya watu mbalimbali kwani lengo ni kuunganisha nguvu katika ulinzi wa misitu iliyopo nchini.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule hizo wamesema wanaipongeza TFS kwa uamuzi wake wa kuona haja ya kutoa elimu inayohusu utunzaji misitu kwao, kwani kuna mambo wamejifunza na wanaamini yatawasaidia kushiriki kikamilifu kwenye utunzaji misitu nchini.
Wamesema ni kweli wanafahamu faida za misitu lakini elimu ambayo wameipata kutoka TFS wamebaini kuna mambo mengi ambayo hawakuwa wanayajua lakini sasa wamepata mwanga huku wakitumia nafasi hiyo kuomba mafunzo hayo yawe endelevu na sio kwao tu bali na kwa wengine kwani wote wanajenga Tanzania moja na kwamba misitu ni uhai.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam wakiwa ndani ya msitu wa asili wa Pugu ambapo lengo la ziara hiyo ni kujifunza kuhusu uhifadhi wa mazingira lakini msitu huo ndiko unakopatikana mti wa Mpugupugu ambao ndio chimbo la jina la Sekondari ya Pugu
Moja ya mti mrefu uliopo ndani ya msitu wa asili wa Pugu
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani na Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kuwapeleka kwenda kushuhudia vivutio vilivyomo kwenye Msitu wa asili wa Pugu
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakionesha furaha yao baada ya kufanya utalii wa ndani kwa kwenda Msitu wa Asili wa Pugu .
Baadhi ya wanafunzi wakishangilia baada ya kufika juu ya kilele cha Mlima wa Pugu ambapo walitembea kwa saa moja na nusu hadi kufika keleleni
Hivyo makala TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU
yaani makala yote TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tfs-yapeleka-elimu-ya-utunzaji.html
0 Response to "TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU"
Post a Comment