Loading...

OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza

Loading...
OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza
link : OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza

soma pia


OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wakala wa Afya wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) imesema kuwa OSHA imekuwa sehemu ya watu wengine kujifunza kutokana na utoaji wa huduma sehemu za kazi.

Akizungumza na waandishi habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa OSHA Joshua Matiko  wakati wa ugeni wa Wizara ya Kazi ,Uwezeshaji ,Wazee,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipotembelea  OSHA kwa ajili ya kujifunza utoaji wa usalama wa afya mahala Pa Kazi.
Matiko amesema kuwa nia ya OSHA ni kuwa Taasisi kubwa ya watu kujifunza masuala ya utendaji mahala pakazi na kuweza kupata tija.

Amesema kuwa serikali ya mapinduzi kuja kujifunza licha ya kubadilishana mawazo inaunganisha udugu uliopo kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Matiko amesema kuwa Zanzibar kwenda kujifunza sio peke yao bali hadi taasisi za nje zimefika kujifunza na kwenda kwao kuunda chombo kama OSHA.Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kutokana na kutoa elimu kwa ajili kumepungua kwa magonjwa na majanga mahala pakazi kutokana na elimu wanayoitoa.

Nae Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman amesema kuwa OSHA wana vitu vizuri ambapo tukienda  kufanyia kazi tutaweza kupata mabadiliko katika mahala pakazi. Shadia amesema kuwa licha ya kujifunza ni pamoja na kuishauri serikali kuanzisha wakala inayojitegemea ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo, Wanawake ,Habari ,Utalii na Vijana Mwantatu Mbaraka Khamis amesema OSHA imezatiti katika kulinda usalama wa afya mahala pakazi kutokana na utendaji wake pamoja na kuwa  wataalam wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Afya wa Usalama Mahala Pakazi (OSHA) Joshua Matiko akizungumza kuhusiana na ugeni kutoka Zanzibar kujifunza katika wakala huyo.
 Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee ,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman akizungumza kuhusiana na ujio wao katika Wakala wa Afya wa Usalama Pahala Pakazi (OSHA) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee ,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya Bunge na Kaimu Mkurugenzi OSHA.


Hivyo makala OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza

yaani makala yote OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/osha-yawa-taasisi-ya-wstu-wengine.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza"

Post a Comment

Loading...