Loading...

Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi

Loading...
Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi
link : Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi

soma pia


Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

 Rais Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Nanyamba, Tandahimba, na Newala Mkoani Mtwara kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya uhakika ili kuunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kujiletea maendeleo yao.

Akizungumza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, Rais Magufuli amesema Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Nanyamba yenye urefu wa kilometa 50 itakayogharimu kiasi cha Tsh.bilioni 86 na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe kutangaza zabuni ya ujenzi wa kilometa zingine na kufikia kilometa 100 na hivyo kuunganisha kwa urahisi nyanda za kiuchumi katika mikoa ya kusini.

“Barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha uchumi mikoa ya kusini, hatuwezi kushindwa kujenga kilometa 100, lengo letu kuu ni kuiunganisha Bandari yetu ya Mtwara na mizigo inayotoa Malawi,” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa katika kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara, ambapo Serikali imetekeleza ununuzi wa korosho kutoka kwa wananchi wenye korosho zaidi ya kilo 1500, na Tsh Bilioni 50 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao, na kwa upande wa wakulima wa korosho wenye kilo chini ya 1500 wamelipwa kiasi cha Tsh Bilioni 578.

Rais Magufuli amewahiza wafanyabiashara walanguzi wa zao la korosho ‘Kagomba’ kuacha kuwadhulumu wakulima wadogo kwa kuwapa bei ambayo hailidhishi huku wakijua wametumia gharama kubwa katika kuendeleza zao hilo, na kusema serikali ya Awamu ya tano haitarudi nyuma kuwatetea wakulima hao.

“Utakuta mtu amelima korosho zake, amenunua madawa, ametumia gharama kuzivuna unakuja kumpa bei ya 1500, kwa Serikali ya Awamu ya Tano hili halikubaliki”, alisema Rais Magufuli.

Akiongelea miradi mingine inayotekelezwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Mtwara, , upanuzi wa uwanja wa Ndege na ukarabari wa mradi wa maji wa makonde ambao utagharimu kiasi cha Tsh.bilioni 160 zikiwa ni fedha za mikopo kutoka Serikali ya India unaowezesha ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 nchini.


Hivyo makala Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi

yaani makala yote Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/rais-magufuli-aahidi-kuiunganisha-kanda_3.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi"

Post a Comment

Loading...