Loading...
title : Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi
link : Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi
Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi
Na Woinde Shizza Globu ya jamii
Watoa huduma za msaada wa kisheria nchini wametakiwa kutotumia nafasi yao ya kutoa msaada wa kisheria kufanya mambo kinyume na taaluma yao na maadili yao ya kikazi.
Hayo yamebainishwa Leo na Katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria prof Sifuni Mchome wakati akiongea katika kongamano la Watoa huduma za msaada wa kisheria uliofanyika jijini Arusha ambapo alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watoa huduma hao kufuata maadili ya Kazi yao.
Alisema kuwa kwakuwa Watoa huduma wa msaada wa kisheria wanafanya Kazi kwa kujitolea hivyo ni wajibu wao kuzingatia maadili ,yanayoendana na Katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kulinda tamaduni njema za kitanzania.
"Napenda kusisitiza msitumie mlango wa usaidizi wa kisheria kutumika kama vibaraka " alisema mchome.
Kwa upande wake Waziri wa katiba na sheria Balozi dkt Augustine Mahiga aliwataka Watoa huduma hii ya kisheria kutumia kikamilifu makubaliano yaliowekwa na utekelezaji wake usibaki katika karatasi bali wayafanyie Kazi kikamilifu ili wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria waweze kufaidika nayo.
Aliongeza kuwa itakuwa haina maana kama sheria ,kanuni miongoni na makubaliano yaliopo hayata mnufaisha Mwananchi mhitaji wa huduma hii pia libainisha kuwa wakati pia serikali inaendelea kuimarisha mifumo ni vyema pia wahakikishe wanawafikia wananchi walio wanyonge katika maeneo yao.
Mahiga alisema kuwa serikali iko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wananchi wanyonge wanathaminiwa nakupewa hadhi sawa na wengine ,na kwakutilia mkazo serikali imepitisha sheria ya msaada wa kisheria na itaendelea kuimarisha nifumo ya upatikanaji haki nchini ili huduma hii itolewekatika utaratibu na mfumo mzuri utakao wezesha kuwafikia wananchi kwa wakati na kwa ubora unaostaili.
Aidha aliwataka wasaidizi hawa wa kisheria kuendelea kusimamia misingi imara ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inayotambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kulinda tamaduni njema za kitanzania ambazo ndiyo tunu yetu tunayojivunia katika kulinda utu na heshima ya mtanzania .
Waziri wa katiba na sheria Balozi Dkt Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kufungua kongamano
Msaili wa Watoa huduma za msaada wa kisheria nchi bi.Felistas Mushi akizungumza na Waandishi mara baada ya ufunguzi.
Hivyo makala Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi
yaani makala yote Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/watoa-huduma-msaada-wa-kisheria-waaswa.html
0 Response to "Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi"
Post a Comment