Loading...

RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

Loading...
RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI
link : RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

soma pia


RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetangaza rasmi kuanza kupitia maombi ya vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu mwaka huu ambapo matarajio yao ni kuhakiki vyeti vya wanafunzi 100,000.

Kwa mujibu wa RITA ni kwamba ili mwanafunzi mwenye sifa ya kupata mkopo kwa ajili ya masomo ya vyuo vikuu anapaswa cheti chake cha kuzaliwa kufanyiwa uhakiki ili kujiridhisha na taarifa zake na baada ya kuhakikiwa majibu yanayorudishwa kwa mwanafunzi na kutumwa Taasisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Kendelea na mchakato wa kutoa mkopo.

Hivyo katika kufanikisha wanafunzi wanapata mikopo kwa wakati RITA imeamua kuanza mchakato wa kuhakikiwa vyeti vya kuzaliwa mapema wakiamini itasaidia wanafunzi hao kuwa na uhakika wa taarifa zilizomo kwenye vyeti vyao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam , Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu/ Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Emmy Kalomba Hudson amesema uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi unaanza leo na kuendelea huku akifafanua kuwa moja ya kielelezo au kiambatanisho ambacho kinatakiwa na taasisi ya mikopo ni uthibitisho wa mwanafunzi anayeomba mikopo.

"Hivyo tumeona ni busara kuanza mchakato mapema ili wanafunzi waweze kupata mikopo. Tunajua kuna taasisi nyingi zinahusika lakini kwa upande wetu tumeona tuanze mapema. Kwanini tunahakiki? Tunajua watu ambao tunawasajili wanavyeti lakini lengo ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili kupata mikopo basi wapate," amesema Hudson.

Ameongeza kuwa cheti cha kuzaliwa mwenye mamlaka yenye kuthibitisha uhalali wake ni RITA,na kwa kutambua jukumu hilo wameona ni bora wakaanza mapema na kwamba gharama za kuhakikiwa Sh.3000 huku akitoa rai kwa wanafunzi au wazazi kufungua akaunti email ili kurahisisha kujaza maombi na kutuma RITA yakahakikiwe

"Wale ambao tutahakiki vyeti vyao na kuthibitisha taarifa zao tutawajibu na kisha taarifa zao kupeleka bodi ya mikopo kwa maana wanastahili kupata mkopo na wale ambao taarifa zao hazitakuwa RITA nao watajulishwa ili waangalie namna ya kufanya.

"Pia uhakiki huu mbali ya kuhakiki cheti cha mwanafunzi,tunafahamu wakati mwingine mwanafunzi anaweza kuwa amepoteza mzazi mmoja wapi au wote, na hivyo mwenye kuthibitisha cheti cha kifo ni sisi RITA," amesema na kuongeza ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa mapema ili kuepuka unaoweza kujitokeza mbele ya safari.


Amefafanua zaidi kuwa kuna haja ya kuanza mapema ili kufanya zoezi kuwa rahisi na kupata muda unaofaa na kwamba wanaanza leo na kama mtoto yupo shule wanajua  wazazi wanatunza vyeti, na kama hawana basi ndio muda mzuri wa kufuatilia na kwamba maombi 100,000 ndio ambayo yatahakikiwa kwa mwaka huu.

 Amesema kuwa " Ada ya uhakiki wa maombi ni Sh.3000 tu,mwaka jana tulisikia wanafunzi wametapeliwa kwenye vibanda vya Intaneti, wapo waliotozwa hadi Sh.30,000 na hiyo imekuwa kero.

Wazazi wafungue akaunti wenyewe za email ili kupunguza gharama. Wapo wengine ambao walilipa fedha na maombi yao hayakwenda. Wanafunzi waache kuzembea wajitume kwa kujaza maombi wenyewe. Zoezi hilo ni endelevu na vizuri wakaanza mapema kabla ya muda wa kuomba mikopo haujafika,"amesema Hudson

Hata hivyo amesema maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kwani hiyo itasaidia kupitia.maombi mengi na ndani ya siku tatu wahusika watakuwa wamejibiwa huku akitoa rai kwa makatibu tawala walioko wilayani ambao wanatambuliwa na RITA kuhakikisha wanafunzi wanajaza maombi kwa njia ya mtandao kwani mwaka jana wapo ambao walijaza maombi bila kutumia mtandao na hivyo kusababisha maombi kuchelewa RITA.

Akizungumzia changamoto ambazo zilijitokeza mwaka jana wakati wa uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi, Hudson amesema kulikuwa na changamoto katika upigaji picha wa vyeti ambapo zilikuwa hazionekani kwa uharaka, wengine walikosea nywila(paswadi) hivyo hata majibu yalipotumwa wengine walichelewa kupata kwasababu ya kusahau nywila.

Pia changamoto nyingine kuna wanafunzi wengine walikuwa wazembe maana walikuwa wanajipiga selfie na kisha kutuma Rita,jambo ambalo haliko kwenye utaratibu."Changamoto nyingine wapo ambao walikuwa wamezaliwa nje ya nchi lakini nao wanakuja RITA.Hao tulikuwa tunawapa maelekezo ya namna ya kufanya.

"Kulikuwa na changamoto pia ya mtandao kuzidiwa kutokana na idadi kubwa ya waombaji.Ndio maana tumeanza mapema kuondoa changamoto hiyo.Na baada ya kuona changamoto tumeamua kuboresha mtandao wetu kwa mfano iwapo mwanafunzi atasahau nywila basi Luna sehemu ataiona," amesema Hudson.

Alipoulizwa kuhusu vyeti vyeki,amejibu ni kweli vipo kwa watu wachache ambao wamevipata kutoka kwa wahuni ambao wamekuwa wakitengeneza vyeti feki,view vya kuzaliwa au vya kielimu na vyeti vingine,na wanapobaini wanachukua hatua za kuwafikisha wahusika katika vyombo vingine vya kisheria."Ndio vipo huwa tunaona kwenye televisheni wakionesha watu wamekamatwa na mitambo ya kutengeneza vyeti.Hata hivyo vyeti vyeti vinausalama wa kutosha ."

Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini kuna mtu au watu wanatengeneza vyeti.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria Lina Msanga amesema kinachohakikiwa na RITA ni cheti cha kuzaliwa au cheti cha kifo na sio matangazo,hivyo kinachotakiwa kutumwa RITA ili kihakikiwe ni cheti.
 Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu /Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Kalomba Hudson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam wakati akitangaza kuanza uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wanaojiandaa kujiunga na masomo ya elimu ya juu ambao wanasifa za kupata mkopo
Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria kutoka RITA Lina Msanga akifafanua jambo kuhusu uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi wanaosubiri kupata uhakiki wa mkopo baada ya RITA kuthibitisha taarifa zao

 


Hivyo makala RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

yaani makala yote RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/rita-kuanza-uhakiki-wa-vyeti-vya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI"

Post a Comment

Loading...