Loading...
title : TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM
link : TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM
TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM
Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV
Mkazi wa Singida, Mariam Rajab Juma anayesumbuliwa na tatizo la kidonda kikubwa kilichopo sehemu ya mgongoni ameeleza kuwa tatizo hilo chanzo chake kilianzia kwenye Jipu ambalo baadae lilipasuka nakupelekea kidonda hiko.
Mariam aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) amezungumza hayo alipokuwa akihojiwa na Waandishi wa Habari hospitalini hapo.
Mariam ameeleza kuwa tangu kufika Muhimbili ameona kuna mabadiliko makubwa, amesema kwa sasa anatembea vizuri tofauti na zamani.
"Naishukuru Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa hali niliyonayo sasa, kuna mabadiliko makubwa tangu tatizo hili lianze miezi Saba iliyopita", amesema Mariam.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma amethibitisha kuwepo kwa Mgonjwa huyo takriban wiki moja iliyopita, amesema wamefanya uchunguzi kwa Mariam nakujiridhisha kile kinachomsumbua.
Dkt. Mkoma amesema baada ya upembuzi yakinifu kuhusu kinachomsumbua Mariam, ataendelea na matibabu katika hospitali ya Ocean Road kwa muda na baadae atafanyiwa uchunguzi tena na Jopo la Madaktari.
Amesema baada ya uchunguzi huo, Jopo hilo la Madaktari litakaa tena kufanya tathmini kujua anaendelea na matibabu ya aina gani.
Kuhusu tatizo zaidi lilonalomsumbua Mariam, Dkt. Mkoma amesema suala hilo litabaki kuwa siri kati ya Madaktari na Mgonjwa.
Hata hivyo, Dkt. Mkoma ametoa wito kwa Wananchi kuwa na tabia yakuchunguza afya mara kwa mara, amesema inapokea kuwa na kidonda chochote kwenye kovu la zamani lazima kufanya kipimo kujua ni aina gani ya kidonda.
Hivyo makala TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM
yaani makala yote TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tatizo-langu-lilianzia-kwenye-jipu.html
0 Response to "TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM"
Post a Comment